ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 12, 2013

ADHABU YA MAREFA SAANYA NA ONESMO, YAONYESHA KWAMBA YANGA NI TIMU YA WANANCHI

Imeandikwa na Baraka Mbolembole
Mtu ‘ mkubwa’ ni mwanafunzi, kwani huona mbali zaidi na kwa kuona kwake huko hutamani vitu zaidi kuliko watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba mtu huyo hata kama atakuwa na uwezo wa kuona mbali zaidi, au awe na akili nyingi zaidi, ukweli hawezi kubadili mwendo wa historia. Kitu ambacho anaweza kufanya ni kubadilisha matukio Fulani. Ni kutokana na mambo kama haya ndipo viongozi wakubwa hutokea.
Fasihi ni taaluma, Taaluma ni elimu, na elimu ni maisha. Mtu huzaliwa na akili. Katika makuzi yake, mtu husikia, huona, huonja, hunusa na hutenda. Vitendo hivi ndiyo msingi wa kutumia akili ili kupata elimu. Hivyo elimu ya kwanza na sehemu kubwa na sehemu kubwa ya elimu ya maisha hupatikana nje ya darasa. ‘ Yaani, Maisha kutokana na vionjo vya mwili’ . Tunajifunza ili tuishi, na katika maisha yetu tunakutana na marafiki wa kila aina, kwa wanasoka maisha yao mengi hutumia kutengeneza marafiki wa dhati kutoka katika family ya soka. Urafiki ni Uadui, au Uadui ni Urafiki?
Dunia hadaa. Kwa mtu ambaye hajawajhi kufika pwani na kuiona bahari, anaweza kudanganywa kuwa maji ya bahari ni ‘mekunde’. Kama ni rahisi, mtu huyo anaweza kudanganyika kuwa maji ya bahari ni mekundu. Hatari ya uongo siku zote iko wazi. Itatokea siku mtu huyo ‘ mjinga’ asiyeijua bahari, akajifunga na kufanya safari ili aje kuhakikisha uwepo wa maji mekundu ya bahari. Apatapo ukweli na kubaini kuwa alidanywa, mtu huyo atamuamini tena mtu aliyempatia habari hizo hata kama atakuwa akizungumza ukweli wakati mwingine.


Usaliti kwetu sisi mashabiki upo siku zote, Martin Saanya, na aliyekuwa mwamuzi wake msaidizi, Jesse Onesmo wamekutwa na adhabu ya kufungiwa kutochezesha soka kwa muda wa mwaka mmoja. Waamuzi hao walichezesha mchezo kati ya Yanga na Coastal Union, septemba 28 na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Waamuzi hao, wenyeji wa mkoani Morogoro wamefungiwa kwa kuwa walishindwa kuendana na kasi ya mchezo na kujikuta wakifanya makosa ya mara kwa mara. Adhabu ya kiki ya penati ambayo Saanya aliitoa kuelekea katika lango la Yanga, dakika ya mwisho ya mchezo na kutengeneza matokeo ya sare ndiyo iliyowaletea matatizo, na kupelekea wakapata adhabu kubwa. Sifikirii kama angepewa adhabu hiyo kama angetoa wakati Yanga wakisaka bao la kusawazisha. Waamuzi hawa ni kweli waliboronga, na mechi ilikuwa kubwa kwao. Lakini ukichunguza hatua kwa hatua ambazo walizitumia kufanya maamuzi na kuusimamia mchezo ule, utagundua kuwa makosa waliyofanya yalikuwa ni ya kibinadamu, na mkwaju wa ' utata' wa penati kwangu mimi nauchukulia kama sehemu ya kawaida ya mchezo wa soka.
NI,KWELI, SAANYA, ONESMO WALIBORONGA, lakini adhabu walizopewa ni kama ziliandaliwa. Sijui ni wapi lakini nakumbuka wakati Fulani nilikutana na Mwamuzi, Othman Kazi, kiukweli nilitaka kujua kwa nini alifungiwa. Akaniambia kuwa kuna watu walikuwa hawamtaki kwa sababu wanazozijua wao. Kina, nani hao? “ Nasubiri muda wao madarakani umalizike ndiyo nitarudi kuchezesha tena soka” aliwahi kuniambia Kazi, ambaye aliwahi kukutwa na adhabu kubwa ya kufungiwa kwa kosa alilodai kuwa si la kweli. Alifungiwa kwa madai ya kupokea hela kutoka mahali Fulani waawakati Fulani mjini Bukoba. Aliniambia mambo mengi sana kuhusu kazi yao ya uamuzi na matatizo ya ubinafsi yaliyopo katika chama chao. 
Wakati mwingine ni lazima chama cha waamuzi kiwasemee waamuzi hasa wanapokutana na adhabu ambazo zinakuwa ni kali zaidi na ambazo zinaweza kuwafanya wakashindwa kuaminiwa tena, hata pindi watakaporudi uwanjani baada ya adhabu kumalizika.
Kitu, gani ambacho kimemfanya Saanya, na Onesmo wahukumiwe? Ni kuiadhibu Yanga katika ‘muda mbaya’, nafikiri tu kama adhabu ile ingetolewa katika lango ya Coastal mambo yangekuwa makubwa kiasi hiki. Hapana, LAKINI imekuwa tatizo kubwa hadi katika kazi yake, kwa kuwa aliamua mkwaju wa penati. Katika mechi kama ile, katika muda kama ule, katika kipindi ambacho timu nzima ya Coastal ilikuwa ikicheza katika eneo la hatari la Yanga, ilikuwa ni lazima Saanya ‘ afunike mkono wake’ haijalishi mpira ulimgonga mahali gani Haruna Niyonzima. Yanga walikuwa wakiomba mechi imalizike na presha ya Coastal ilikuwa juu kuliko muda wowote ule wa mchezo.
Adhabu yake ni fundisho kwa waamuzi wote ambao huishia kuchezesha mechi kwa namna wanavyopangiwa na watu au vile watakavyo wao. Soka letu haliwahitaji waamuzi ‘ wazembe’, soka letu haliwahitaji waamuzi kama Saanya ambao hawawezi kuendana na kasi ya mchezo, soka letu linawahitaji waamuzi kama Saanya ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi makubwa, na kuyasimamia maamuzi yake. Mechi kubwa tatu, zimemuondoka katika sifa za mwamuzi bora nchini, hii ni kutokana na uzoefu wake mdogo katika uchezeshaji mechi kubwa, lakini ana kitu ambacho waamuzi wengi hawana. 
Watu wengi wa mpira nchini hawana ujasiri wake wa kukubali kupoteza kazi yake kwa sababu alisimamia maamuzi ya kuiadhibu Yanga katika mechi kubwa, tena ikicheza na timu kutoka mkoani, ndani ya uwanja wa Taifa.
Viongozi wetu ‘wakubwa’ wa soka wana elimu nzuri ya darasani, lakini ni waongo na wanaosimamia upande mmoja, tu. Jana niliandika makala kuhusu timu yate ya taifa kuwa na wachezaji wengi wa Simba, Yanga, na Azam. Nilisema ni sawa tu wala haina tatizo timu hizo kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars. Lakini ubora wao hauwezi kuletwa kwa njia ya upendeleo uwanjani, wanatakiwa wapambane na washinde kwa nguvu zao wenyewe, kwa mbinu zao wenyewe, na mwisho wa siku mwamuzi anatakiwa kusimamia mchezo kwa kufuata utaratibu na sheria zake. 
Hakuna, mkubwa kuliko mwamuzi katika mchezo wa soka, ndiyo maana Ufaransa ilifuzu kwa kombe la dunia, 2010 baada ya goli la ‘ mkono la Thierry Hennry, ndiyo maana, Bao la ‘ mkono wa mungu’ la Diego Maradona dhidi ya England, 1986 litabaki kuwa sehemu ya kumbukumbu za fainali za kombe la dunia, ni kama shuti kali la Frank Lampard dhidi ya Ujremani, katika ‘ WOZA 2010’.

Soka linahitaji matokeo yale, ( Yanga v Coastal) “ Niliwaona baadhi ya wachezaji wetu wakiwa walelala chini, niliwaambia ‘ okoteni mpira nyavuni’. Sikuwa tayari, kukata tama. Hutakiwi kukata tama hadi sekunde ya mwisho. HII NDIYO SABABU SOKA NI MCHEZO WA KUVUTIA” aliwahi kusema aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uturuki, Faith Terem mara baada ya timu yake kuitupa nje ya robo fainali ya Euro 2008 timu ya taifa ya Croatia, wakiwa wamefungwa bao dakika ya 119, lakini wakasawzisha dakika ya 1119, lakini wakasawzisha dakika ya 120 na kushinda kwa mikwaju ya penati. Adhabu ya Saanya kwangu mimi ni kuzidi kuthibitisha kuwa ‘ Yanga ni timu ya wananchi’ lakini isiyojua thamani yake.

No comments: