ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 2, 2013

Anatafutwa na polisi kwa kosa la kumlawiti na kumharibu mwenziye baada ya kumlewesha


JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.

Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.

“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile
pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha kupoteza fahamu,” alisema.

Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile. Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.

“Raia wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.

Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.

Hillary Shoo, TANZANIA DAIMA, Singida.

4 comments:

Anonymous said...

Sawasawa hii ndio dawa ya kuacha ulevi kudadeki. We mtu utalewaje mpaka upoteze fahamu?? Huyo alikuwa anatafuta sababu tu

Anonymous said...

Wewe mdau hapo juu una laana .

Anonymous said...

Aisee!huyo rafiki alikua ana nia mbaya toka mwanzo coz vile viroba vya jogoo ni vikali kama gongo na vinakwaruza koo yani konyagi inasubiri sana...sasa anamnunulia tisa!khaa,ndo kashampa kilema ila somo amelipata

Anonymous said...

Tanzania bwana sijui mtajifunza lini baada ya kuweka picha ya mtu anaye tafutwa mnaweka bendera ndiyo maana watu hamwapati kwasababu mnawaficha wenyewe.