Tabasamu: Gareth Bale ametangazwa leo kuwa mchezaji wa Real Madrid
Akibusu jezi: Bale hakupoteza muda kuwaonesha mashabiki wa Madrid kuwa ni mtu wa ushindi
Bosi wa ukweli: Bale amesema licha ya yeye kuwa ghali zaidi, bado anatambua kuwa Ronaldo ndio mtu muhimu zaidi Bernabeu
Si mchezo: Maelfu ya mashabiki wa Madrid wamemtazama Bale akitambulishwa
Nyomi iliyojitokeza kushuhudia nyota huyo akitambulishwa rasmi.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
LICHA ya kuwa mchezaji ghali kuliko wote duniani, Gareth Bale ametambua na kuweka wazi kuwa Cristiano Ronaldo ndiye “Bosi” katika klabu ya Real Madrid.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24-ametangazwa kuwa mchezaji wa Bernabeu leo asubuhi kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya dunia ya pauni milioni 86 akitoka klabu ya Tottenham.
“Cristiano kwangu mimi ni mchezaji bora wa dunia na yeye ndio sababu ya mimi kufanya maamuzi ya kujiunga hapa”. Alisema Bale. “Sidhani kama nahitaji kumsaidia Cristiano kuwa mcheza bora wa dunia kwa sababu ameshakuwa tayari”
No comments:
Post a Comment