Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar,akiongea wakati wa hafla ya chakula cha jioni ilioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangia kampeni ya "Dawati kwa kila mtoto" Inayoendeshwa na taasisi hiyo, alieketi ni mwenyekiti wa Bank M, Bw, Nimrod Mkono(MB) akisikisilza kwa makini wakati wa shughuli hiyo, zaidi ya Shilingi Milion 200 ziliweza kuchangiwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar,akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Joseph Warioba pamoja na Mh. Jaji Augustine Ramadhani na Mh. Salim Ahmed Salim wakati wa hafla ya chakula cha jioni ilioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangia kampeni ya "Dawati kwa kila mtoto" Inayoendeshwa na taasisi hiyo.Hafla hiyo ilifanyika Septemba 27,2013 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo wakati wa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununulia Madawati kwa shule za msingi nchini.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Wairoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Majaar Trust Balozi Mwanaidi Majaar wakati wa hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni ya “Dawati kwa kila mtoto” inayoendeshwa na taasisi hiyo.
1 comment:
Mama tunakumisss hapa DC!! This is what we want in Tanzania. Let make a difference to those unprivileged individuals than calling political parties meeting every other month na kufunguwa matawi if all Tanzanians start from here DC, MD VA contribute $10 EACH hata hospitali tungeweza kuinua hali yake au tukajenga vyoo mashuleni watu wanateseka sana huko Nyumban, wanafunzi hawana madawati shule hazina vyoo!!!! Huu ni mfano wa kuigwa sana! Hongera mama!
Post a Comment