ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 26, 2013

JK: Wafadhili tupeni fedha za MDG`s

Rais Jakaya Kikwete, amewataka wabia wa maendeleo wa nchi maskini kutimiza ahadi zao kama njia ya uhakika kuhakikisha Malengo ya Milenia yanayolenga kuzitoa nchi maskini kwenye uduni na kuziharakishia maendeleo.

Aidha, amesema Tanzania itatekeleza kwa ukamilifu baadhi ya malengo, lakini itakuwa vigumu kuyatelekeza yote manane kama inavyotakiwa chini ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2015.

Aliyasema hayo alipozungumza kwenye mkutano uliojadili jinsi ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia, New York, Marekani juzi.

Mkutano huo uliandaliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Benki ya Dunia (WB) kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Rais Kikwete alisema kukawia kwa wafadhili hao kutoa fedha za utekelezaji wa malengo, kumechangia kwa kiasi fulani utekelezaji huo kutokuwa na kasi iliyotarajiwa kutokea mwanzo.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema pamoja na kucheleweshwa kwa fedha za kutosha za utekelezaji, Tanzania itaweza kwa kiasi fulani kufanikisha utekelezaji wa baadhi ya malengo, lakini ni dhahiri kuwa malengo mengine hayataweza kufikiwa ifikapo mwaka 2015 ambao ndiyo mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa Malengo hayo.

Aliyataja Malengo hayo kuwa ni kufuta umaskini uliokithiri na njaa, kuinua kiwango cha afya na kupunguza vifo vya akinamama na watoto na kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira endelevu.
CHANZO: NIPASHE

3 comments:

Anonymous said...

Mmh hatuhitaji pesa. Tatizo letu ni leadership kwenye ngazi zote. Timu yetu haina tatizo la vifaa, ni kocha. Mmenipata?

Anonymous said...

For sure

Anonymous said...

tuoeni fedha, tupeni fedha, tupeni fedha, mpaka lini Tanzania