ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 3, 2013

KUKIWA NA SHUGHULI LADHIMA KUWE NA MAJAMVI JE KUVAA SHANGA NI UREMBO?

watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu,
nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..
kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..
kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..
wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..
sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....

4 comments:

Anonymous said...

Shanga hazina kabila, ila zaidi mvaaji anajua kutumia, rangi zina maana yake lakini la muhimu ni jinsi shanga ilivyokukaa kuna bana tumbo, kidaka Athumani kichwa wazi na appetizer kila aina ina kazi yake unapokuwa kwenye shughuli haya tena kazi kwako .............

Anonymous said...

Haina maana yoyote ni ulimbukeni tu,zamani walikuwa wanavaa sababu ni urembo maana walikuwa hawana nguo za kusitiri mwili mzima,ndio ikaja idea ya shanga kama urembo ulivyo kama cheni au bangili. Kina dada zetu wa sasa wanajivalia tu na hawajui ni hasa maana yake.

Anonymous said...

Takriban inafahamika na weledi wengi kwamba umbo la mwanamke ni lenye uzuri wa pekee kimaumbile.

Kunoga kwa uhondo wa tendo la ndoa ni kutayarisha mazingira ya kusisimua. Huvaa na huvaliwa wenye kujua thamani ya penzi shada la Maua na shanga za kila aina na rangi sawia.

Wako wenyekukogeshwa kwa maji asumini na maua ya waridi. Wakafukiziwa udi au manukato Perfume de Paris France. Ama kilua na mkadi.

Wasojua maana hawaambiwi maana. Kaeni na ushamba wenu. Mufe na utamu wenu kama mua.

Zanzibar.

Wasoju

Anonymous said...

Hazina issue