Msomaji wa makala haya yenye kichwa kinachosema “Makosa 10 ambayo wanawake huyafanya faragha”, wiki iliyopita niliweza kufafanua kosa la kwanza ambalo ni udanganyifu wa hisia, yaani ufeki wa mambo.
Simama katika ukamilifu wako, toa mrejesho sahihi kwa mwenzi wako. Kama hujisikii burudani, mpasulie ya moyoni na kama anakupatia vilivyo mwelekeze katika eneo ambalo kwa hakika akilifanyia kazi inavyotakiwa basi itakuwa bam bamu.
Wanawake wengi ni waongo, wanafeki hisia lakini hiyo huwatesa wenyewe, kwani baada ya kuchushwa, huamua kutoa siri za faragha zao kwa marafiki au kutafuta wataalamu wa mapenzi. Mbaya zaidi ni kwamba hao walalamikaji wanakuwa hawajawahi kuzungumza kinagabaubaga na wenzi wao. Tuache zama za ujima, twende kisayansi.
Mwili ni wako, maeneo murua ndani yako unayajua mwenyewe. Mshirikishe mwenzio ili kuufanya muunganiko wenu uwe mzuri. Siku zote kemea udanganyifu, simamia kilicho sahihi. Kuna faida yingi zitafuata kwako kama tu utaacha kufeki.
KUONESHA NA KUSEMA
Tukio la wewe na mwenzi wako kukutana faragha, unatakiwa kulipa thamani ya aina yake. Kipengele cha kwanza nimekutaka usipende kufeki mambo, hiki hapa kinakuelekeza wewe kujiachia. Onesha hisia zako waziwazi na uzungumze ukweli wa kilicho ndani yako.
Wanaume siyo wafalme njozi, kusema wana uwezo wa kusoma na kuelewa hata mambo yasiyoonekana. Kama ambavyo wewe ulivyo na kikomo cha kuelewa hisia za mwenzi wako ikiwa hakuoneshi na hafunguki kwa maneno, vivyo hivyo na yeye.
Kwa maana hiyo, wanaume hawana uwezo wa kuzisoma fikra zako kama kivitendo huoneshi wala hutamki. Kama husikii raha, husisimki, huduma yako haikufikii inavyotakiwa, ububu wa nini? Ukimya wako utamuweka mwenzi wako katika mazingira magumu ya kukuhudumia.
Vilevile ukimya wako utakuumiza zaidi kwa sababu anayehitaji huduma bora ni wewe, lakini hutoi mwangaza jinsi ambavyo ungependa uhudumiwe. Baadaye utalalamika kwamba mwenzi wako hakufikishi. Hapo mwenye makosa ni wewe na tafsiri ni kwamba mateso yako ya kugandwa na ‘maugwadu’ umejitakia mwenyewe.
Usiogope kusema ukweli. Huyo uliyenaye kitandani ni mwenzi, mwandani, msiri wako, kwa hiyo hutakiwi kumficha kitu chochote. Usifanye makosa ambayo wengi wanayatenda, wanashindwa kuwaambia ukweli wapenzi wao kisha wanakwenda kumwaga mtama kwa marafiki.
Mwambie mwanaume wako kipi ufanyiwe. Je, hakuandai inavyotakiwa? Funguka mama, huo ni uwanja wenu wawili, tena maalum sana. Pengine ili ufurahie huduma ya faragha ni lazima uhudumiwe kwa mtindo wa kuelekea ‘mjini’, sasa usipomwambia yeye atajuaje?
Yupo ambaye ili aone uzuri wa faragha na afike kileleni, sharti kuu lazima denda lichukue nafasi. Mwingine husisimka na kuhitimisha safari yake kikamilifu kama mtoa huduma ataweka mkazo kifuani, yaani pale anavyofyonza vile vidude viliwili vya kifua, ndiyo inakuwa raha na burudani kwa asilimia 100.
Itaendelea wiki ijayo
GPL
No comments:
Post a Comment