ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 17, 2013

Mnigeria akamatwa Kenya na dawa za kulevya, inaaminika alipitia airport ya Julius Nyerere


Raia wa Nigeria aliyefukuzwa nchini Kenya kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya amekamatwa jijini Nairobi na inaaminika amepitia kwenye airport ya Julius Nyerere na kupitia mpaka wa Namanga. Enobemhe Emanuel Peter amekamatwa na pakiti 425 za Heroin huko jijini Nairobi. Mnigeria huyu ni moja kati ya watu waliofukuzwa nchini Kenya kwa agizo la Rais Uhuru Kenyatta kuwafukuza watu wote wanaojihusisha na biashara za dawa ya kulevya.
Idara ya uhamiaji Tanzania wamesema “Mtu akifukuzwa na nchi moja haimaanishi kwamba haruhusiwi kuingia nchi nyingine. Kama jirani zetu wangekuwa na ushirikiano na sisi baada ya kumkata mtu,wangetupa taarifa ili anapoingia Tanzania tunakuwa makini naye. Huyo mtu alipita tu hapa Tanzania”. So, haijulikani kama mtu huyo alipita airport ya Julius Nyerere na hizo dawa au la.
Imeripotiwa na gazeti la Mwananchi

1 comment:

Anonymous said...

Tanzaniaaaa ingenious mfano wa Kenya! Yeyote atakaye kama tea na madawa ya kulevya asiye raia wa Tanzania, fukuzia mbaali kabisa na kwa Watanzania funga miaka 20-30 bila dhamana yeyote wala mjadala. Mpaka kieleweke. Wanatuharibia Amani na nchi kwa ujumla.