Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtangaza Mhariri wa Picha wa zamani wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi, kuwa Balozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.
Hamisi, ambaye aliwahi pia kuwa mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited kama Mpigapicha, alipata ajali mbaya mwaka 2008 na kupooza sehemuya mwili.
Katika uteuzi huo uliotangazwa na Waziri Nchimbi jana, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani litamtumia Hamisi kutoa elimu na hamasa kwa Watanzania kuepuka ajali kwa kuwa zina madhara makubwa kwa maisha ya binadamu.
Aidha, Waziri Nchimbi alisema ajali za barabarani zimeendelea kuwa janga linalogharimu maisha ya watu wengi, hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuzidhibiti.
Alisema hayo jijini jana alipokuwa akizindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2,012, jumla ya watu 17,820 wamekufa katika ajali za barabarani.
Miongoni mwao ni abiria 5,237, watembea kwa miguu 5,771 na madereva 1,292. Vifo vilivyotokana na ajali 98,693 za barabarani, kuna waendesha pikipiki 2,887, waendesha baiskeli 2,385 na wasukuma mikokoteni 245.
Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti, mwaka huu, ajali 15,682 zimetokea na kusababisha vifo 2,541 na majeruhi 13,752. Kati ya ajali hizo, pikipiki ni 5,433, ambazo zilisababisha vifo 704 na majeruhi 4,312.
“Hali hii ya matukio ya ajali za barabarani inatisha. Lazima tuchukue hatua madhubuti kukabiliana nazo kwani zinapoteza maisha ya watu wengi na kusababisha ulemavu wa kudumu na hivyo kupunguza nguvu kazi ya taifa,” alisema Waziri Nchimbi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment