Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi.Anna Magoha wakati akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora katika sherehe za Mei Mosi Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mwaka jana
Katika salamu hizo, Rais amemuelezea Bibi Magoa kuwa alikuwa kada na mchapakazi hodari ambaye ameacha pengo kubwa katika Chama na Serikali.
“Kwa hakika umepoteza moja ya nguzo zako mkoani Tabora. Bibi Anna amekua kada na mtumishi wa kutumainiwa katika Chama chetu cha Mapinduzi na serikali kwa ujumla. Tumeondokewa na mtu muhimu na mchapa kazi hodari” Rais amesema na kumuomba Bibi Fatma Mwassa kumfikishia salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki zake wote.
Rais pia amewatumia salamu za pole wafanyakazi na wananchi wa Urambo ambao marehemu amekuwa akifanya nao kazi tangu alipohamia Wilayani humo Mwaka 2010.
Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike na wajukuu wawili. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Mkoani Iringa kwa maziko.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam, Tanzania
25 Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment