Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.
Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.
Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.
Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.
Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.
Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi
1 comment:
nalaani sana tukio hili la kigaidi kama lilivyotokea huko westgate na watu wasio na hatia wakauawa na wengine kujeruhiwa. hata hivyo napenda kutoa maoni kwa tathmini nilioifanya ni kwamba ushughulikiaji wa tukio hili ikiwemo mapambano na magaidi SERIKALI YA KENYA inayoongozwa na Rais UHURU KENYATTA imeonesha udhaifu mkubwa katika mpambano huo, hii serikali ilikataa kusaidiwa kupambana na magaidi mara tu shambulio lilipotokea. taarifa walizokuwa wakizitoa nyingi sio za kweli, serikali hiyo ilikuwa ikijitapa itawamaliza magaidi hao lakini ushindi umeekuwa ni wa magaidi, kwa siku nne jeshi battalion nzima iliolizunguka mall hilo ilishindwa kuwasaga saga magaidi na mwishowe wakatoroka,na bado serikali hii inazidi kusema uongo tu na kuzidisha kiburi. kwa tukio kama lile sidhani kama walihitaji battalion ya kijeshi. walihitaji makomandoo wa kupambana na wale magaidi 15 huku mall likiwa limezungukwa na polisi kuhakikisha gaidi hapati nafasi ya kutoroka.kwenda na vifaru tanks za kivita ni dalili ya uoga wa kijeshi. huyu uhuru Kenyatta si ajiuzulu tu badala ya kuendelea kuongopa na kuzidisha kiburi.poleni sana mlioathirika na shambulio hili.
Post a Comment