THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tuwasaidie
Wacongo, wamechoshwa na vita – Rais Kikwete
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka
Jumuia ya Kimataifa kufanya kila linalowezekana kumaliza mzozo wa kisiasa na
mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ili kutoa nafasi kwa wananchi wa Congo kuishi katika amani
na kujitafutia maendeleo.
“Hawa
ni watu walioteseka sana na kwa muda mrefu, wana haki ya kupata amani, wana
haki ya kupata muda wa kupumzika kutokana na vita na mapigano,” Rais
Kikwete ameuambia mkutano wa pili wa wakuu wa nchi zilizotia saini mkataba wa
kutafuta amani, usalama na ushirikiano katika DRC chini ya Umoja wa Mataifa (UN).
Katika
mkutano huo, uliofanyika leo, Jumatatu, Septemba 23, 2013, kwenye Umoja wa
Mataifa mjini New York chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu wa UN, Mheshimiwa Ban Ki Moon kama
ulivyokuwa mkutano wa kwanza uliofanyika Februari 24, mwaka huu, 2013, mjini
Addis Ababa, Ethiopia, Rais Kikwete amewaambia viongozi wenzake wa nchi
wanachama wa Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)
na wengine waliotia saini mkataba huo:
“Nadhani
hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuhusu DRC ni nzuri na mchakato wa kutafuta
amani nchini humo unakwenda vizuri. Ni muhimu tukafikia mwisho wa tatizo hili
kwa sababu wananchi wa DRC wametesema mno na kwa muda mrefu. Wana haki ya
kupata amani, wana haki ya kupata muda wa kutosha wa kufanya mambo ya maana
kama ya maendeleo yao badala ya kukaa na kufikiria vita,”
Rais Kikwete amesema kwenye mkutano huo.
Rais
Kikwete amesema kuwa siri ya kufanikiwa katika DRC ni kutekeleza yale yote
ambayo nchi hizo zimekubaliana kutekeleza katika DRC akisisitiza: “La
msingi ni kila mmoja wetu kutekeleza yale yote tuliyokubaliana. Hiyo ndiyo siri
ya kuleta amani na utulivu katika DRC.”
Mbali
na Rais Kikwete, mkutano huo wa leo umehudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa
Uganda ambaye pia ni Mwenyekiti wa ICGLR,
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Rais Joseph Kabila Kabange wa DRC, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais
Joyce Banda wa Malawi ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU)
Mheshimiwa Nkosazana Dlamini-Zuma, na Katibu Mkuu wa UN ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo.
Aidha,
mkutano huo umehudhuriwa na Makamu wa Rais na wawakilishi wa Jamhuri ya Congo
(Congo-Brazzaville), Zambia, Angola na Sudan Kusini.
Kwenye
mkutano huo, wasemaji wengi wamesisitiza kuwa hakuna amani ya kweli katika DRC
na nchi za Maziwa Wakuu bila viongozi wa nchi hizo kukubali kuzungumza na
kukubaliana na vikundi mbali mbali ambavyo vinapigana dhidi ya baadhi ya nchi
hizo.
Baadaye
leo, Rais Kikwete amehudhuria mkutano wa Baraza la Uongozi la Umoja wa Kutafuta
Usalama wa Chakula na Ushirikiano wa Grow
Africa uliofanyika kwenye Ofisi za Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF)
uliofanyika kwenye ofisi za taasisi hiyo katika Marekani mjini New York.
Rais
alizungumza kwa ufupi katika mkutano huo ambako alitaka wafadhili wa miradi ya
kilimo katika Afrika kuongeza kasi ya kutoa fedha za kuleta mageuzi ya kilimo
katika Bara la Afrika kwa sababu kila mmoja wa wadau anatekeleza majukumu yake
kwa haraka zaidi kuliko wafadhili.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23
Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment