Advera Senso
Matukio ya watu, wakiwamo viongozi wa dini, watalii na wafanyabiashara kumwagiwa tindikali, yameliamsha Jeshi la Polisi, ambalo limetangaza kufanya uchunguzi ili kubaini vimiminika vya tindikali vinavyoingizwa, kusambazwa na kuuzwa nchini kama vimezingatia sheria.
Uchunguzi huo unaoanza mara moja, unafanywa na Jeshi hilo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutumia kikosi maalumu cha kuzuia uchochezi na ugaidi.
Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso, alisema hayo jana kupitia taarifa aliyoituma kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms).
“Kufuatia vitendo vya baadhi ya watu (wahalifu) kuwamwagia wenzao tindikali, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutumia kikosi maalum cha kuzuia uchochezi na ugaidi limejipanga kuwafuatilia watu wote wanaoingiza, kusambaza na kuuza vimiminika vya tindikali endapo wanazingatia sheria zilizowekwa dhidi ya vimiminika hivyo,” alisema Senso na kuongeza:
“Atakayebainika kwenda kinyume, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.”

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Kwa kifupi Jeshi la Police limeshindwaaaaa kuwajibika kabisa!!!!! Kazi ni kula Rushwa tu! Wana nuke Rushwa mpaka wamesahau utekelezaji wa kazi zao! Inasikitisha sana hakikaaa. Kila kukichaaaa matukio yamekuwa mengi Mpaka wananchi tunaogopa hata kutokana nje, hakuna Penney usalama, Benki kunatisha uvamizi Kila kukichaaaaa! Barabarani kuna Tindikali sasa wananchi turned waapi? Police wamejisahau na wamesahau wananchi wamejali posho na Rushwa ......
Post a Comment