Shirikisho la kimataifa la soka FIFA limetoa viwango vya ubora wa timu za taifa vya kila mwezi huku vikiwa na mabadiliko kadhaa yanayoashiria kupanda na kushuka kwa viango kwa baadhi ya timu .
Viwango hivyo vinaonyesha kuwa timu ya taifa ya Hispania imeendelea kuongoza ikiwa kwenye nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina ambao wamepanda kwa nafasi mbili toka nafasi ya nne kwa mwezi uliopita .
Hispania wameshikilia nafasi ya kwanza kwa karibu miaka mitatu wakiwa na rekodi ya matokeo mazuri kwenye asilimia kubwa ya michezo yake rasmi ya kiushindani na ile ya kirafiki.
Nafasi ya tatu na ya nne zimekwenda kwa Ujerumani na Italia huku Colombia ikikamilisha orodha timu tano bora duniani .
Timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo imezidi kupanda kiwango ikiwa kwenye nafasi ya 6.
Ubelgiji ambao kwa sasa wanajivunia kuwa na kundi la wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu wanaounda timu yake ya taifa imepanda kwa nafasi nne toka nafasi ya kumi kwa mwezi uliopita wakiwa mbele ya Uruguay na Brazil zinazoshika nafasi za saba na nane .Brazil wamepanda toka nafasi ya tisa huku Uruguay wakiwa wamepanda kwa nafasi tano toka nafasi ya 11 .
Orodha ya timu kumi bora inakamilishwa na timu za Uholanzi na Croatia zinazoshika nafasi ya tisa na nafasi ya kumi . Uholanzi wameshuka kwa nafasi nne toka nafasi ya tano mwezi uliopita na Croatia wameshuka kwa nafasi mbili .
England wamezidi kushuka viwango kwa sasa wako kwenye nafasi ya 17.
Timu ya taifa ya England imeendelea kushuka kadri siku zinavyozidi kuongezeka wakiwa kwenye nafasi ya 17 toka nafasi ya 13 . England waliwahi kufikia mpaka nafasi ya tatu mapema mwaka huu lakini kutokana na matokeo mabovu ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata imeendelea kushuka kwenye viwango vya ubora .
Tanzania iko kwenye nafasi ya 127 duniani sawa na nafasi ya 37 kwa bara la Afrika.
Kwa bara la Afrika viwango hivyo vinaonyesha kuwa timu ya taifa ya Ivory Coast inashika nafasi ya 19 ikiwa imeshuka toka nafasi ya kumi na nane ikifuatiwa na Ghana ambayo imeshika nafasi ya 24 kama ilivyokuwa mwezi uliopita .
Algeria , Nigeria na Mali zinakamilisha orodha ya tano bora huku Cape Verde wakizidi kupanda wakiwa kwenye nafasi ya sita . Misri , Burkina Faso , Cameroon,Senegal na Afrika kusini bzinamalizia top 10 ya bara la Afrika huku Tanzania ikiwa kwenye nafasi ya 37 kwa Afrika na 127 kwa Dunia ambapo imepanda kwa nafasi moja
Algeria , Nigeria na Mali zinakamilisha orodha ya tano bora huku Cape Verde wakizidi kupanda wakiwa kwenye nafasi ya sita . Misri , Burkina Faso , Cameroon,Senegal na Afrika kusini bzinamalizia top 10 ya bara la Afrika huku Tanzania ikiwa kwenye nafasi ya 37 kwa Afrika na 127 kwa Dunia ambapo imepanda kwa nafasi moja
No comments:
Post a Comment