Simon Sirro
Mkuu msaidizi wa oparesheni hiyo, Simon Sirro, alisema jana kuwa kati ya wahamiaji waliokamatwa, Warundi ni 4,229, Wanyarwanda 1,446, Waganda 647, Wakongo 443, Wasomali 42, mmoja kutoka Yemen na Mhindi mmoja.
Kamanda Sirro alisema kati ya silaha hizo zilizokamatwa bunduki aina ya SMG ni nne, magobole 15, Short gun moja, Mark4 moja, na Rifle moja. Kuhusu risasi ni SMG 163, gobole 82, Mark4 risasi 20, mabomu sita ya kutupwa kwa mkono na mitambo miwili ya kutengeneza magobole.
Aidha, alisema katika operesheni hiyo zimekamatwa sare za jeshi zinazohofiwa kuwa ni za jeshi la Burundi na kuwa jumla ya majambazi 32 wamekamatwa, wote ni raia wa Tanzania.
Alisema wahamiaji 2,377 wamerejeshwa kwao kwa maamuzi ya mahakama, 1,866 wamerejea kwa hiyari, 396 wameachiwa huru na 2,170 wanaendelea kuhojiwa.
SOURCE: NIPASHE
1 comment:
Kwa hiyo wakimbizi TZ wapo Kagera na Kigoma peke yake ? Kama kuna wakimbizi haramu wamejazana Dar sio Kigoma
Post a Comment