Bendera ya Kenya ikiwa kwenye mzunguko wa Dupont Circle Washington, DC ambapo Wakenya wa DMV walikutana katika kuwakumbuka na kuomboleza waliopoteza maisha kwenye janga la ugaidi lililosababisha vifo 69 na wengine 175 kujeruhiwa kutokana kikundi cha ugaidi cha Al shaabab kuvamia jumba lanye maduka na migahawa la Westgate siku ya jumamosi Sept 21, 2013. Wakenya na marafiki zao wakiwemo raia wa nchi nyingine walijumuika pamoja huku wamewasha mishumaa na kuimba wimbo wa taifa wa Kenya huku wengine wakitia saini kitambu cha rambirambi na kutoa misaada mbalimbali itakayokabidhiwa Red Cross kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa uvamizi huo wa ugaidi wa Westgate.
Bi. Prudence Ukwishatse akiwaongoza wenzake na kuwapa maelekezo kwenye maombolezo yaliyofanyika leo Ijumaa Sept 27, 2013 katikati ya mzunguko wa Dupont Circle uliopo Washington, DC. Jumapili yatafanyika maombolezo mengine Lincoln Memorial iliyopa Washington, DC kuanzaia saa 10 jioni(4pm)
Richard Porter akitoa ratiba ya maombolezo ya Jumapili Sept 29, 2013 yatakayofanyika Lincoln Memorial, Washington, DC
Waombolezaji Wakenya na marafiki zao na watu mbalimbali kutoka mataifa mwengine waliopoteza ndugu zao wakifuatilia maelekezo.
Waombolezaji waliojumuika pamoja leo Ijumaa Sept 27, 2013 wakiwa wameshika mishumaa kwa ajili ya kuwaombea wenzao waliopoteza maisha kwenye janga hilo la ugaidi nchini Kenya.
Juu na chini Wakenya waliojumuika pamoja na marafiki zao wakimsikiliza Bi Prudence Ukwishatse alipokua akiongea.
Sharon Satie akiongoza wimbo wa taifa wa Kenya.
J uu na chini ni Wakenya na marafiki zao na watu wengine toka mataifa mengine wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa taifa wa Kenya.
No comments:
Post a Comment