Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo katika viwanja vya shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya
Kikosi cha timu ya Young Africans kimefanya mazoezi yake ya kwanza mkoani Mbeya katika viwanja vya shule ya sekondari Iyunga jioni ya leo kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Mbeya City katika dimba la uwanja wa Sokoine.
Msafara mkubwa ulijitokeza kukipokea kikosi cha Yanga jana jioni kuanzia maeneo ya kituo cha mafuta cha TAZAMA na kuongozana na mashabiki, wapenzi na wanachama waliojitokeza kuipokea timu mpaka eneo la soweto ilipofikia.
Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara Young Africans wamefanya mazoezi leo kufuatia jana kuwa safarini kutoka jijini Dar es salaam ambapo timu iliwasili majina ya saa 12:30 na kufikia katika hoteli ya Mbeya Paradise Inn iliyopo maeneo ya soweto jijini Mbeya.
Wachezaji wamefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts huku wapenzi washabiki na wanachama wakijoitokeza kwa wingi kukishuhudia kikosi cha watoto wa jangwani ambao wameliteka jiji la Mbeya tangu kufika kwake.
Mara baada ya mazoezi ya leo kocha ameseam kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi na anaamin timu yake itapata ushindi na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.
Aidha viongozi wa Yanga, benchi la ufundi na wachezaji wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapaa kutoka kwa wenyeji Tawi la Yanga mkoani Mbeya ambao wamejitolea muda wao wote kuwa na timu bega kwa bega katika maandaliz ya mchezo huo wa jumamosi.
Kesho majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki timu itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine tayari kabisa kwa kuikabili timu ya Mbeya City siku ya jumamosi.
No comments:
Post a Comment