Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?
Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu!
Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba!
Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake