Wednesday, October 30, 2013

Irene Paul: Anaamini bila Kimombo, Bongo Movie itasota sana

Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni aliingia mzigoni kutengeneza filamu na staa kutoka Ghana, Van Vicker, anasema lugha ina mchango mkubwa katika mafanikio ya filamu. 

Mbali ya hilo, Irene ametumia wasaa aliopewa na gazeti hili kuwaasa Watanzania wakiwamo wasanii wenzake kwamba wawekeze kwenye suala la elimu la hususani lugha ya Kiingereza akisema ndiyo kikwazo kimojawapo kwa baadhi ya vijana kutopata ajira.
IRENE Paul, staa aliyewahi kutamba katika filamu za Kalunde, Saturday Morning, Kibajaji, Love & Power, Handsome wa Kijiji na nyinginezo nyingi, amesema ndoto ya filamu za Tanzania kutamba Afrika haitatimia kama waigizaji wake wataendelea kutumia lugha ya Kiswahili tu.
Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni aliingia mzigoni kutengeneza filamu na staa kutoka Ghana, Van Vicker, anasema lugha ina mchango mkubwa katika mafanikio ya filamu.
“Sitaki kusema watu waache kuigiza filamu za Kiswahili, ninajua kwamba tuna wateja wengi Bongo na pia ni wajibu wetu kuhakikisha lugha yetu inakua,” alisema.
“Lakini hatupaswi kuufumbia macho ukweli kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotupaisha kimataifa.”
Mbali ya hilo, Irene ametumia wasaa aliopewa na gazeti hili kuwaasa Watanzania wakiwamo wasanii wenzake kwamba wawekeze kwenye suala la elimu la hususani lugha ya Kiingereza akisema ndiyo kikwazo kimojawapo kwa baadhi ya vijana kutopata ajira.
“Sasa hivi baadhi ya ofisi zetu zimetawaliwa na watu kutoka nchi za jirani, hata sisi wasanii baadhi yetu tunashindwa kuvuka mipaka huku lugha hiyo (Kiingereza) ikiwa ni kikwazo,” anasema na kuongeza.
“Ni wakati wetu Watanzania kujikita katika suala hili, pia hata kwa wasanii wenzangu. Wenzetu wa Nigeria, Ghana na kwingineko wanatamani kufanya kazi na sisi, lakini wakijaribu kuangalia filamu zetu na lugha tunayoitumia wanapata wakati mgumu japokuwa ni lugha ya taifa.”
Akizungumzia suala la waigizaji kugeukia kazi ya kuongoza filamu, Irene, anasema kwamba kamwe hawezi kuwa mwongozaji wa filamu kama ilivyo kwa wasanii wengi wenye majina, badala yake kazi hiyo anawaachia watu wengine ili kila kazi anayoifanya iwe na umakini na utaalamu zaidi.
Kuna tabia imejengeka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo kujivika madaraka mengi yakiwamo ya mwongozaji, mtayarishaji na mwigizaji katika filamu moja.
Anasema hali hiyo inasababisha umakini katika utayarishaji wa filamu kupungua.
“Mimi nimeamua kuwa chachu ya mabadiliko, nimeona bora nimuite mtaalamu wa kuongoza afanye kazi yake, mtayarishaji naye afanye kazi yake ili mwisho wa siku, macho na mawazo ya wengi yaweze kuzaa kitu ambacho kitasaidia kusukuma ubora wa kazi zetu,” alisema.

Bado aiota Devil’s Kingdom

No comments: