Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon mwezi Septemba mwaka huu wakati wa Mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu ametuma salam za rambirambi kwa Familia na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha Mlinzi wa Amani Mtanzania ambaye amepoteza maisha siku ya jumapili baada ya kushambuliwa na kundi la waasi la M23 katika eneo la Kiwanja- Rushuru kilimita 25 magharibi ya mji wa Goma. katika shambulio hilo, Mlinzi mwingine ambaye pia ni Mtanzania amejeruhiwa. kumekuwapo na mapigano kati ya Majeshi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) na Kundi la M23.
Luteni Rajabu Ahmad Mlima Enzi ya Uhai Wake
Na Mwandishi Maalum
Kwa mara
nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani
vikali tukio la kuuawa kwa
mwanajeshi wa kitanzania aliyekuwa akihudumu katika Misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kutuliza Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO)
Kifo cha mwanajeshi huyo mtanzania kimetokea jana jumapili baada ya
kushambuliwa na kundi la M23 ambalo linapigana na majeshi ya Serikali ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya KONGO ( FARDC)
Katika salamu zake
rambirambi kwa familia ya marehemu
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu
huyo wa Umoja wa Mataifa, ameelaani vikali mauaji hayo na kuahidi
kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea
kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua
zote muhimu kuwalinda raia wa DRC
“ Ninalaani vikali mauaji ya mlinda amani kutoka Tanzania ambaye
alishambuliwa na kundi la M23 katika
eneo la Mashariki ya DRC, ninatoa
salamu zangu za rambirambi kwa familia
ya marehemu, na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ” ananukuliwa Katibu Mkuu akisema.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoufikia Uwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, siku
ya jumapili , zinaeleza kwamba Mlinzi huyo wa amani aliyepoteza maisha na ambaye jina lake linahifadhiwa kwa
sasa anacheo cha Luteni na kwamba alishambuliwa wakati kikosi chake kikiwa katika harakati za kutoa
ulinzi wa raia katika eneo la Kiwanja- Rutushura kilomita 25 kutoka Magharibi mwa
mji wa Goma.
Katika mashambuli hayo mlinzi mwingine wa amani ambaye
pia ni mtanzania amejeruhiwa.
Aidha taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa, inaeleza kwamba
Umoja wa Mataifa utachukua hatua zote
muhimu kwa mujibu wa Azimio namba 2098 ( 2013 ) kutimiza wajibu wake .
Ni kupitia Azimio hilo ambalo lilipitishwa mwezi
Marchi mwaka huu, Baraza
Kuu la Usalama liliridhia kuanzishwa kwa Brigedi Maalum ( FIB) ambayo
pamoja na mambo mengine imepewa jukumu
la kutumia nguvu pale inapobidi ikiwa ni
pamoja na kuwapokonya silaha makundi ya wanagambo wenye silaha likiwamo
kundi hilo la M23 na makundi mengine
ambayo yamekuwa yakiendesha mapigano na machafuko katika DRC.
Mapigano yanayoendelea hivi sasa kati ya majeshi ya serikali ya Kongo na kundi la M23
yamefuatia kuvunjia hivi karibuni kwa mazungumzo ya Kampla
yaliyokuwa yakiendelea kati ya
pande mbili. Hali inayolifanya eneo hilo
la Mashariki ya Kongo kuzidi kuwa tete.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake