Sunday, October 27, 2013

MSIBA WA MARTHA SHANI UMEWAGUSA WENGI AKIWEMO BALOZI MULAMULA

Rev. Nicodemus Hanje akiongoza Ibada ya msiba wa Martha Shani iliyofanyika Jumapili Oct 27, 2013 Greenbelt, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka kila kona na kudhihirisha jinsi gani msiba huu ulivyowagusa wengi na katika historia ya Ubalozi wa Tanzania chini ya Balozi Liberata Mulamula wafanyakazi na maofisa wa Ubalozi huo wamechanga na kununua tiketi tatu za ndege za mume na watoto wa marehemu na kuwawezesha kusafiri kesho Jumatatu Oct 28, 2013 asubuhi na Ethiopia Airline kwenda Tanzania kwa mazishi, mwili wa marehemu utaondoka siku ya Jumaane Oct 29, 2013.
Rev. Nicodemus Hanje akimpa pole mume na watoto wa marehemu kwenye ibada ya kumuombea Martha Shani iliyofanyika Greenbelt, Maryland.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kuwashukuru Watanzania kwa kuwa kitu kimoja na kuwezesha kufanikisha kuchangisha fedha kipindi cha wiki moja na kuwezesha kumsafirisha marehemu Tanzania kwa mazishi pia Balozi Mulamula aliwakilisha rambi rambi ya Mhe. Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara kwa wafiwa.
Mtoto wa marehemu, Joseph Kassuwi akiwaeleza Watanzania waliofika kwenye Ibada ya mpendwa mama yake maneno aliyoambiwa na mama yake kabla ya pumzi yake ya mwisho alisema mama yake alimuambia amtunze mdogo wake kabla hajamalizia alishindwa kujizuia akaanza kububujikwa na machozi na kufanya watu waliofiak kanisani hapo nao kushindwa kuvumilia.
Wachungaji na maaskofu wakiwaombea familia ya marehemu.
Mume wa marehemu Alex Kassuwi akijaribu kuelezea historia ya yeye na marehemu walivyokutana na jinsi gani walivyokuja Marekani lakini hakuweza kumalizia historia yao baada na yeye kuanza kulia kwa uchungu baada ya kusema yeye na mke wake walikuja Marekani kutafuta maisha baada ya kusema maneno hayo alishindwa kuendelea na kuanza kulia kwa uchungu huku akisaidiwa na Tino Malinda kwenye picha kulia.
DMK kulia akiwatuliza familia ya marehemu waliposhindwa kujizuia na kutokwa na machozi .
Mariam Mtunguja akisoama wasifu wa marehemu kwani yeye alimjua marehemu tangia walipokua na miaka sita. na marehemu alipokuja Marekani na familia yake walifikia nyumbani kwake kabla ya kuanza maisha yao.
Familia ya marehemu wakitoa heshima zao kwa mpendwa wao mwisho wa ibada ya kumuombea mama yao na mke wa Alex Kassuwi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa heshima zake kwa marehemu.
Baada ya watu wote kumaliza kutoa heshima zao kwa marehemu, mume wa marehemu alimvisha pete mpendwa mke wake.
Familia ya marehemu wakiwasha mshumaa kwa pamoja wakati wa chakula cha pamoja.
Mhe. Balozi Liberata Mulaula pamoja na maafisa Ubalozi na Rais wa Watanzania DMV wakifuatilia Ibada
kwa picha zaidi za msiba huu bofya soma zaidi





12 comments:

  1. Asante sana lukas kazi nzuri sana mungu akulipe kaka yetu ubarikiwe
    Dada lao

    ReplyDelete
  2. poleni wanafamilia kwa kuondokewa na mpendwa wenu Martha Mungu awape nguvu Mume wa marehemu, watoto na familia Mungu alitoa na ametwaa jina lake libarikiwe.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wanaFamilia Mungu awatie nguvu. Inasikitisha sana jamani . R.I.P Martha

    ReplyDelete
  4. hivi ndivyo inavyotakiwa kupigi picha msibani,sio unampiga picha marehemu uso halafu wanazitandaza mitandaoni,sio ustaarabu kabisa

    ReplyDelete
  5. Poleni sana kwa familiar na jamii kwa huu msiba wa ghafla. Mungu awape nguvu wakati huu. Sio rahisi lakini jipeni mwoyo.Tutazidi kuwaweka kwa maombi. Jane Akola musi.

    ReplyDelete
  6. kweli ni ngumu sana kukubaliana na hii hali ila Mungu ndio wakuwapa faraja ya moyo.

    ReplyDelete
  7. Kweli Mungu akupe nguvu baba na watoto kwa kipindi hiki kigumu sana kwenu ila Mungu ndio muweza wa yote...sijui huko nyumbani wapo kwenye hali gani kupokea huu msiba mzito wakuondokewa na mpendwa ghafla.

    ReplyDelete
  8. NIMEFIWA NA MAMA YANGU NAE PIA NI GHAFLA NIKIWA MKUBWA NISEME MTU MZIMA NA UCHUNGU BADO NINAO KWANI NATAMANI ANGEZIDI KUWA NAMI,LKN NIKIRUDI KUANGALIA HAWA WATT WALIOACHWA NA MAMA YAO WAKIWA WADOGO SANA NI MACHUNGU ZAIDI...KWELI MUNGU ANAMAKUSUDI YAKE KWA MWANADAMU,JINA LAKE LIBARIKIWE SANA.

    ReplyDelete
  9. POLENI SANA MUNGU AWAPE NGUVU NA MSAFIRI SALAMA NA MRUDI SALAMA JINA LA MUNGU LIBARIKIWE KWANI YEYE NDIYE MUWEZA WA VYOTE.

    ReplyDelete
  10. Ni wakati mgumu sana Baba na watoto kuondokewa na mama gafla! hata angekuwa ameumwa mngekuwa na wazo kwamba tumejaribu ila tumeshidwa, yaani kutoka kazini kama kawaida na kufika nyumbani anafariki nafikiri kusahau kifo chake itakuwa ngumu sana.Mwenyezi anaye juwa maisha yetu azidi kuwatia nguvu sana.

    ReplyDelete
  11. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIBARIKIWE MILELE NA MILELE NA MILELE!!!!!!!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake