Advertisements

Wednesday, October 23, 2013

MUUZA CHIPS AMTEKA MTOTO TANDALE DAR...ATOKOME BILA KUJUA ANAENDA KUMFANYIA NINI MTOTO HUYO

MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie.
Mama mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’.
Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi. 
Mtuhumiwa wa utekaji.Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa kuwa mtekaji ambaye alishaacha kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka muda mrefu na binti yao na hakukuwa na dalili za kurejea.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani. 
Baba mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.Inadaiwa kuwa katika mawasiliano hayo, mtekaji alikataa katakata ombi la kumtaka amrudishe mtoto wao na kutaka apewe kiasi cha shilingi milioni 6 ili kutekeleza jambo hilo ingawa baadaye ilibainika jamaa huyo alikuwa Gairo mkoani Morogoro.
Wazazi hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji alishtukia na kukimbia.

No comments: