ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 19, 2013

RAIS KIKWETE ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WABENA MKOANI NJOMBE

Rais Jakaya Kikwete akipokea Mkuki wakati akisimikwa Uchifu wa Kabila la Wabena na mmoja wa wawakilishi wa Wazee wa Kabila hilo,kwenye wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Wazee wa Kabila la Wabena wakimsimika Uchifu Rais Jakaya Kikwete.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiteremka Jukwaani baada ya kusimikwa Uchifu wa Kabila hilo na kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Njombe.
Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mkewe Mama Salma Kikwete baada ya kusimikwa Uchifu wa Kabila la Wabena,wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Pongezi zikiendelea.
Machifu wa Kabila la Wabena wakiwa kwenye picha ya Pamoja.


kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Shangwe zilitawala wakati Rais Kikwete akibonyeza kitufe cha kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
Rais Kikwete akizindua Vitabu.
Mamia ya Wakazi wa Mkoa wa Njombe wakiwaangalia vijana wa Halaiki wakati wakitoa Burudani uwanjani hapo.
Viongozi mbali mbali.
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha Wageni kwenye Banda la Sido wakati apokuwa akitembelea mabanda mbali mbali kwenye Maonyesho ya Uzinduzi wa Mkoa mpya wa Njombe.
Mmoja wa Watangazaji wa Redio akirusha Matangazo ya moja kwa moja kutokea Mkoani Njombe.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiangalia ngoma kutoka kwa vijana.
Rais Kikwete akisalimiana na Maafisa wa Sido
Rais Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa TBS.
Rais Kikwete akitembelea Mabanda mbali mbali

No comments: