ARUSHA: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha UongoziMwenyekiti wa chama hicho
Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai
ya kukihujumu chama hicho.
Taarifa ambazo zimetufikia hivi
punde kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini,
kinaendelea kufanyika katika Hotel ya Corridor Stream mpaka usiku huu, zimedai
uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa
kwa vielelezo kadhaa na vya Mwigamba na yeye kukiri kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa
ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa
likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii.
Hakuna kiongoi ambaye amekuwa tayari
kuzungumzia suala hili kutoka na kuwa ndani ya kikao hicho ambacho kinaendelea,
lakini Taarifa za uhakika ambazo zimepenyeshwa kwa Mwandishi wa Mabadiliko.com
toka ndani ya kikao hiho zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka.
“Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi
kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba
siyo kiongozi, nadhani tamko litatolewa baadaye,” alieleza mmoja wa wajumbe wa
kikao hicho kinahoendelea Arusha na
kuongea kuwa katika Kompyuta yake baadhi ya maandiko ambayo yamekuwa
yakikikashfu chama yamekutwa ikiwa ni pamoja IP address ya Jina na Maskini
Mkulima ambalo limekuwa likituma post ndani ya Jamiiforums kukuta zinafanana.
Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga
na mtandao wa www.jamiiforums.com mnamo
Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27
ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari wito kwa wana CHADEMA wote.
Makala hiyo ambayo ndiyo
imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa
cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’, inaeleza haya;
Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya
habari namadhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa
wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa
juu wachama.
Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda
zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr.
Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi
chama kinaenda kwa matukio.
Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila
mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki.
Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.
Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia
kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa
ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na
ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali
yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu
Zitto utakuwa ndo mwisho wake.
CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi,
CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama
kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za
serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha
zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini?
Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake
hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo
ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?
Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti
wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana
wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia
mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana.
Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni
ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na
haki ya kilamwanachama.
Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika
katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa
atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na
kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada
yapo hawezi kugombea tenakatika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi
viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili
hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba
bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani,
Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama
nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha
upinzani. Kakichukua kikiwana wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha
miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake
CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi
wa raslimali, katiba mpya,nk.
Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na
tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa
Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele
akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama
mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani.
Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga
chini uchaguzi ujao.
Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na
fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa
chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta
wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia
kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu
mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:
1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006
hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa
zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa
chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo
yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa
makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki
kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza
kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na
wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa
chama.
Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha
kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama
unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe
alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo
kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri
Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila
mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na
wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote
atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.
2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama
zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Kkatibu
Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana
hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha
ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa
2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote
yenye fedha.
Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano
mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua
kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya
namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi
hayo hayajatekelezwa ipasavyo.
Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni
mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo
nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwamfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye
zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising
events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi
kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya
fedha ni questionable.
3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna
kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na
matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua
mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo
agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri
tukiendelea na hawa watututafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala
kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada
kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata
fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara
na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za
kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni
la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi
kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi
fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata
uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini
hawaonekani kama wamejifunza chochote.
5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa
na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya
sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe
wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali
kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya
magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa
katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu
wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi
tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki
zote za M4C.
Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80
ambazomwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka
jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo
hayoyote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya
kiutendajiambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na
kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?
6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza
vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama
kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya
kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa
muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana
kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu. Napenda kwanza kuipongeza kamati
ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala
ama upinzani.
Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi
kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali
za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni
hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama
huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.
Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu
kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa
mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe
matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la
kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama.
Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na
Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi
wetuwakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli
piakwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika.
Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na
hapondipo mtakapojua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo
na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.
Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza
tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.
Ahsanteni kwakunisoma!
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake