Citizen TV Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye nyumba moja huko Mwembe tayari.
Mwanamke huyu nadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.
Taarifa inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.
Mmoja wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’
No comments:
Post a Comment