ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 31, 2013

HALI SI SHWARI UWANJA WA TAIFA KATIKA MCHEZO WA SIMBA NA KAGERA SUGAR MUDA HUU

Mshambuliaji wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Betram Mwombeki, akikokota mpira kuwatoka mabeki wa Kagera Sugar, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara unaoendelea muda huu kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Simba inaongoza bao 1-0 lililofungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 45, baada ya pasi nzuri kutoka kwa Betram Mwombeki.

Katika Mchezo wa Ligi kuu ya Bara Nichini Tanzania kwenye mchezo unaoendelea Muda huu kati ya Simba na Kagera unaochezwa katika Dimba la Uwanja Wa Taifa hali si Shwari mashabiki waanza kungoa viti na Mpaka sasa Mtu Mmoja anashikiliwa na Polisi

Sababu za Vurugu hizo ni Kutoka na Refa Kutoa Penati kwa Timu ya Kagera Sugar dakika ya tisini, Penati hiyo iliyotinga Nyavuni na kupelekea Matokeo Kuwa Simba 1 vs Kagera 1 yamepelekea Mashabiki Kuanzisha Vurugu

Mpaka sasa Polisi Wanaendelea Kutuliza ghasia katika uwanja wa taifa

No comments: