Tunanpenda kuwakaribisha kwenye ibada ya Misa Takatifu kwa lugha ya kiswahili itakayofanyika siku ya Jumapili Novemba 3 katika Kanisa Takatifu la Mtakatifu Edward, Baltimore
Maryland.
(Saint Edward Roman Catholic Church 901 Poplar Grove St,
Baltimore, Maryland 21216 ) (map)
Saa nane kamili mchana (2:00 PM)
Nia ya ibada ni "Kutoa Shukurani na Kuziombea Familia Zetu", Pia Kwa vile Novemba ni Mwezi wa kuwakumbuka
Marehemu, Tutawakumbuka marehemu wetu. Tunaomba Majina toka kwa wote wanaotaka Marehemu wao
wakumbukwe. Tutawaombea wote wanaoomboleza na kuwapa Baraka.
Kwa mawasiliano tumia anuani pepe wauminiwakatoliki@gmail.com
Karibuni sana tafadhali wakaribishe ndugu na jamaa zako.
No comments:
Post a Comment