ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 27, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR.

 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Amin na Linah wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta kwa pamoja usiku wa kuamkia leo,ndani ya viwanja vya Leaders club jijini Dar
 Baadhi ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Amin na Barnaba wakiimba kwa pamoja mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
 Pichani juu na chini ni mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).   
 Mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba kwa hisia huku akipiga kinanda jukwaani usiku wa kuamkia leo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
 Mmoja  wasanii wa kike wa bongofleva aitwaye Recho, ambaye mara nyingi amekuwa akifananishwa na msanii aliyewahi kuwika kwenye anga ya muziki huo Ray C,pichani kati akilishambulia vilivyo jukwaa la fiesta na madansa wake.
 Mwanamuziki wa Bongofleva,Recho akiimba na mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C usiku wa kuamkia leo kwenye jukwaa la fiesta 2013,ambapo muonekano wake uliwashtua wengi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii H Baba akitumbuiza usiku wa kuamkia leo mbele ya mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta linaloendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini  Dar,ambapo mashabiki kibao wa tamasha hilo wanaendelea kumiminika.
 Sehemu ya mashabiki wakishangweka.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013.
PICHA ZAIDI INGIAMICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

No comments: