ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 4, 2013

Azam, Mbeya City presha

Timu ya Mbeya City
Azam FC players
Timu ya Azam FC

Dar es Salaam. Kocha wa Azam, Stewart Hall  amekiri kwamba Mbeya City  ni timu tishio msimu huu, lakini amesisitiza atatumia utaalamu wake wote kuhakikisha anaibuka na ushindi wakati wa mchezo baina ya timu hizo.
  • Azam na Mbeya City zitashuka uwanjani kuumana katika pambano la kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu litakalopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi.
Timu hizo kila moja ina pointi 25 katika msimamo wa ligi, lakini Azam inakamata uongozi wa ligi kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hall akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana alisema:”Mbeya City ni timu nzuri na hakuna anayeweza kupinga, lakini nataka uelewe kwamba mimi si kocha wa kubabaisha ni mtaalamu, amini  mechi itakuwa ngumu lakini nitawafunga.
“Nimeiangalia Mbeya City mara mbili, hapa Dar es Salaam ilipocheza na  Simba pia kule Mbeya ilipocheza na Coastal, ni wepesi yaani kocha wao anastahili pongezi, lakini wana upungufu wao ambao ndiyo nitautumia kuwafunga.
Naye kocha Juma  Mwambusi wa Mbeya City alipotafutwa ili azungumzie tambo za Stewart alisema:
“Mwache aongee, lakini mimi nachojua mpira ni dakika 90, naiheshimu Azam kama moja ya timu nzuri, lakini hatuwahofii kwani hata sisi tunataka kukaa kileleni.
“Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba mechi hiyo itakuwa nzuri sana yaani unaweza kuifananisha na fainali.”
Mwananchi

No comments: