Michuano ya Chalenji itafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji.
Michuano ya Chalenji itafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
Kikosi kamili cha Kilimanjaro Stars kinaundwa na makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia,Kenya) na Aishi Manula (Azam).
Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Katika hatua nyingine, wapinzani wa Kilimanjaro Stars kwenye michuano hiyo, Zambia ‘Chipolopolo’ imeanika kikosi chake kitakachoshiriki michuano hiyo kama nchi mwalikwa.
Chipolopolo inaundwa na makipa Joshua Titima, Toaster Nsabata, Charles Mutanga na Davy Kaumbwa.
Mabeki ni Lawrence Chungu, Christopher Munthali, Jimmy Chisenga, Bronson Chama, George Chilufya na Salulani Phiri.
Viungo ni Roderick Kabwe, Kondwani Mtonga, Shadreck Malambo, Bruce Musakanya, Misheck Chaila, Emmanuel Chimpinde, Julius Situmbeko, Mathews Nkowani, Sydney Kalume na Felix Katongo,wakati washambuliaji ni
Shadreck Musonda, Reynold Kampamba, Festus Mbewe, Patson Daka, Justin Zulu, Alex Ng’onga na Bonwell Mwape.
Wakati huo huo, pambano la kimataifa la Kirafiki kati ya Taifa Stars na Zimbabwe limeingiza Sh 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952. Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Boniface Wambura alisema mgawanyo wa fedha hizo ulikuwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)Sh 7,776,610.17,gharama za uchapaji tiketi Sh3,682,560,asilimia 15 ya uwanja Sh 5,928,124 na asilimia 20 ya gharama za mechi Sh7,904,166.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment