ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 4, 2013

DKT. SENGONDO MVUNGI ALIVYOJERUHIWA VIBAYA, ALAZWA MOI

Dkt. Sengondo Mvungi, akiwa kwenye gari la kubeba wagonjwa, baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akihamishiwa hapo kutoka Hospitali ya Tumbi, Kibaha Jumapili Novemba 3, 2013.
KAMISHNA wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania (CRC), Dkt. Sengondo Mvungi, amelivyojeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na usoni, baada ya kukatwa mapanga, nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji, majira ya saa sita usiku Jumamosi Novemba 2, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na Polisi, Dkt. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, mkoani Pwani, alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua nini kilichokuwa kikiendelea kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu hao ambao walitishia kumuua endapo asingewapa fedha.


Taarifa zinasema, watu hao sita wengine wakiwa nje ya nyumba kwa nia ya kujihami endapo wangevamiwa na majirani, walivamia nyumba hiyo yenye ghorofa moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi wakati huo Dkt. Mvungi akiwa kwenye chumba tofauti katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wavamizi walipoona mke wa Dkt. Mvungi anachelewa kutekeleza maagizo yao, walifyatua baruti na hapo Dkt. Mvungi akajaribu kuelekea kulikotokea mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga ya kichwani na usoni.

Uchunguzi wa awali wa polisi umeonyesha kuwa tukio hilo ni la kihalifu, kwani watu hao ambao kwa sasa wanatajwa kama majambazi, waliiba fedha, simu na laptop, hali inayoonyesha wazi kuwa nia yao ilikuwa ni kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.

Habari kwa hisani ya K-VIS Blog

1 comment:

Anonymous said...

Wewe vipi Dj? Habari ya toka majuzi unaiweka leo. tulishaisoma kitambo, naona blog inakaribia ukingoni