MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.
WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.
MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
-Global Publishers
5 comments:
sijasema katika comment zangu kwamba atatolewa si mnaona wenyewe mnacheza na watoto wa wakuu wa nchi hii wanafanya na kuvuruga watavyo halafu masikini za mungu ndo wanasingiziwa eti magaidi etc ujingu mtupu mnazani watu vipofu mummy niunganishiye na mimi deal nibebe sembe nikikamatwa wakuu watakuja kunitoa
Kama mnamuachia huyo mwanamama muachieni tu na kama mnamchukulia sheria kwa Kuuza hicho mlichomkamata nacho Kama in sembe au bamia au unga wa ulezi au ngano baasi muachieni msituvuruge akili na kutuchanganya na wala msitake kutufanya sie wajinga, tafadhali sana! Tuacheni sie wananchi tunamengi ya kujenga Taifa na sio kutuyumbisha na kesi yenu hiyo na kujidai mnapeleleza Mara mnajadiliana Mara haikuwa sembe ilikuwa unga wa muhogo Mara alikamatwa na dawa ya kunguni blah blah blah !!! Tuacheni sie msitubumbazeeee! Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake.,.
Kama mnamuachia huyo mwanamama muachieni tu na kama mnamchukulia sheria kwa Kuuza hicho mlichomkamata nacho Kama in sembe au bamia au unga wa ulezi au ngano baasi muachieni msituvuruge akili na kutuchanganya na wala msitake kutufanya sie wajinga, tafadhali sana! Tuacheni sie wananchi tunamengi ya kujenga Taifa na sio kutuyumbisha na kesi yenu hiyo na kujidai mnapeleleza Mara mnajadiliana Mara haikuwa sembe ilikuwa unga wa muhogo Mara alikamatwa na dawa ya kunguni blah blah blah !!! Tuacheni sie msitubumbazeeee! Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake.,.
Jamani eeee tusiumize vichwa vyetu waswahili walishasema mwenye nguvu mpishe.
Duh...Heee eeh si mchezo wallah! Yaani n'toto n'dogo n'zigo huoooooo lumbesa nakwambia!
Naomab mwenye email au simu anipeperushie huku. Eeh nataka kupeleka posa mie! Naahidi kum sponsor na Greencard moja kwa moja toka Afrika. Izingatiwe hii ni doziya rehab ili aachane na hii biashara ya unga wa bajia:-) lol.
Post a Comment