- Mimi nikiwa Mwana CCM na Kiongozi pia wa CCM ngazi ya Taifa na Blogger, naomba kusimama mbele ya Mheshimiwa Mbunge Kapuya na Taifa zima la Tanzania pamoja na wasomaji wangu wote wa Blog na meble ya Mungu, kukubali makosa na kuomba radhi, kwake na kwa Mungu wangu zaidi. Mimi ni mmoja wa watu wa kwanza kuamini hadithi iliyojitokeza hivi karibuni kwamba Mheshimiwa Kapuya amembaka na kumuambukiza Ukimwi na kutishia kumuua msichana wa miaka 14.
- Leo ninaomba kusimama hapa na kusema kwamba hii habari ni uongo na ni uzushi wa hali ya juu sana uliotengeenzwa na msichana mzoefu wa uzushi ambaye kwanza si kweli kwamba ni Mwanafunzi, pili ni Mtumzima mwenye mtoto tayari hata kabla hajakutana na Mh. Kapuya, pia ni muongo na mzushi mzoefu aliyewahi kuwadanganya pamoja na Mkurugenzi wa CRDB Bank, pamoja na kuidanganya TAMWA ambayo iliishia kumuripoti polisi na kuishia kwake kukaa rumande Segerea kwa muda mrefu sana.
- Kwa nini niliaiamini hii hadithi ni kwamba kuna siku mimi binafsi tulikuwa tumekaa faragha na Viongozi wengine Watatu wakubwa wa Taifa ambapo mbunge mmoja aliyedai kuijua kwa undani hii hadithi na kuhusiaka nayo, alianza kutuelezea hii hadithi kwa kutmia details kubwa kubwa sana, binafsi nilikuwa ninamuamini sana yule mbunge mpaka leo nilipothibitisha kwa 100% kwamba hii hadithi haiko sawa either na yeye ni muongo wa makusudi mwenye nia mbaya na Mh. Kapuya au na yeye alidanganywa na huyu msichana, ambaye jina lake kamili ni Hamida as opposed na majina mengi ya uongo ambayo amekuwa akiyatumia kudanganyia watu.
- Ninaomba kuwa wa kwanza kubeba huu msalaba, najua kwamba sio rahisi kueleweka na wengi ambao tulishamuhukumu Mh. Kapuya, lakini ukweli ni kwamba ni hadithi ya kutunga iliyoutngwa na msichana mmoja aliyebobea katika uzushi na uongo wa hali ya juu sana. Majuzi Waziri mmoja ninayemuamini sana katika Serikali ya sasa alinishitua kwamba hii hadithi ni ya uongo niiifuatilie tena, lakini sikuamuamini mpaka leo asubuhi sana nilipopigia sim na gazeti moja maarufu sana la Udaku, walioniambia kwamba hii habari si ya kweli na kwamba wanaye huyu msichana pale ofisini kwao, toka asubuhi mpaka sasa nimekuwa kwenye uhakiki wa hii ishu, na sasa ninasema wazi na tena kwamba:-
NINAMUOMBA RADHI SANA MH. KAPUYA NA NI MATUMAINI YANGU MAKUBWA SANA KWAMBA WALE WOTE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU TUTAKUBALI MAPUNGUFU YETU KAMA WANADAMU NA KUMUUNGAMIA CHINI MUNGU WETU, NI KWELI MH. KAPUYA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HUYU BINTI LAKINI YA HIARI SIO KAMA ILIYOELEZWA NA SI KWELI KWAMBA HUYU BINTI NI MWANAFUNZI, HAPANA ANA MTOTO TAYARI NA PIA ALISHAWAHI KULIDANGANYA JESHI LA POLISI HUKO NYUMA.
- Wale wote tunahusika na media tujifunze tena na hili fundisho, tujitahidi kuwa waadilifu na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruka na hadithi nzito kama hii ambayo inaweza kummaliza mwananchi mwenzetu, au kiongozi bila sababu za msingi wala ukweli.
- AGAIN NI MATUMAINI YANGU KWAMBA WALE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU MHESHIMIWA KAPUYA, TUTAJITOKEZA TENA IN THE PUBLIC NA KUMUOMBA RADHI NA MSAMAHA.
- MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
WILLIAM MALECELA

21 comments:
Ondoa ujinga wako hapa wewe mtu mzima.
Bongo ni bongo ukiwa mtu mkubwa au mtoto wa kigogo utafanya kila ujinga na kuongea pumba, nchi imeoza haki hakuna, na inaendelea kuwa nchi ya wajinga..na kama huyo kapuya mapuya anadai itakuwa waziri mkuu, yap he still will be, AIBU TANZANIA.
I still doubt! The only person knows the truth is Kapuya or Victim. I dont see reason to apologize. "People always want to talk to the owner of a dog and not watcher of a dog"
Samahani lakini, kwani hata wewe research yako inaonekana ina upungufu na haimake sense at all. Hizi allegation ni nzito kiasi kwamba wewe utaalamu wako kama blogger na kiongozi wa juu wa ccm sio ticket enough ya kusema una ushahidi kuwa huyu binti ni muongo. You're just another dude trying to avoid justice to take place for this poor girl. You need to be real and thoughfull before jumping to the conclusion, and please don't make your education a subject in this matter. Usually some kind of allegations are handled with justice or police department by doing deep investigation. so wewe ni nani ktk hizo positions? ok your dad is former prime minister...(from your last name) but that alone doesn't give you authority or put yourself in a position to defend such allegation?.Please let the justice department investigate the issue before you put your face all over the map to defend mr Kapuya.
sawa nimekuelewa,lakini wewe uombe radhi kwa mzee Kapuya,ila usitulazimishe watanzania wote tumuone yule dada ni muongo ila kapuya ni mkweli hilo hapana,na pili kwanini umsemee Kapuya mbona yupo kwanini haji 'FRONT LINE' mwenyewe? Acha sheria ichukue mkondo wake tafadhari huyo dada alishafikisha hilo swala mpaka kwa spika ,lakini mzee kapuya amekuwa mkwepaji , wabunge wengi kama si wote wanalijua swala hilo,Naomba msiwanyanyase hao yatima ,watendeeni haki .
le mtu mzima keshapewa bear moja na kapuya baaaasi kapuya kawa mkareeeeeezzzzzz and sainteeeeezzzz hahaha pole le babuz
Kapuya is innocent until proven guilty, he is a victim of political assasination, kwa mtu mzima huwezi amini zile msg anaweza kweli profesa akaziandika...the big no!!!....no research no right to talk..period!!!
Kinachonishangaza kutoka kwa huyu ndugu anakukuwa short minded kwani
-muongo habakwi
-kuwa na mtoto huwezi kuitwa mwanafunzi.
-sms za Kapuya ziko quite open zikionyesha trend ya the whole story. Ingawa muheshimiwa mwenyewe anajichanganya kuwa simu aligawa.
-kufanya sex kwa makubaliano na minor is still a crime.
lets leave the matter to the judiciary to decide.
Sasa kama viongozi wenyewe ndio kama wewe leo ukipewa uwazir itakuwaje?
Mwache aende mwenyewe media akanushe au ndio sababu nchi yenu?
Tatizo mnatuona waTZ mambulula sana. Sasa na hizo message umechunguza pia?
kuna majibu yako hayaeleweki
1. Unasema mkurugenzi wa CRDB: Tutajie jina lake, tarehe waliyokutana, tawi gani la benki ya CRDB
2. Unasema binti ana mtoto: Mtoto anaitwa nani, ana umri gani, baba yake nani, je unauthibitisho ikiwemo hati ya kuzaliwa ya mtoto?
3. mmewahi kukutana naye; Fine jina lake halisi ni lipi, je unawezaje kututhibitishia kuwa mmewahi kukutana naye?
4: habari iliandikwa na tanzania daima; jf mliiinukuu , je unaomba msamaha wa nini, je vyombo vyote vya habari vilivyosoma habari hii kwenye ufupisho wa magazeti asubuhi vinapaswa kuomba msamaha?
5. unasema tufanye utafiti kwanza kabla ya kumhukumu kapuya; well said , kutokana na maelezo yako hakuna utafiti wowote uliyofanya unaotuthibitishia pasipo shaka kuwa kapuya hakutenda hili jambo. habari zako zote ni zile za nimeambiwa, nimepigiwa simu, mara gazeti la udaku wamesema. hili hapana hapana hapana...
6. Ulipewa taarifa na mbunge na mwingine ni waziri pia. kama kweli umefanya utafiti basi ulipaswa utuwekee majina ya mbunge na waziri. Je wewe unawaamini vipi kuwa walikuambia ni ukweli na siyo uongo?
7. Ni "methodology" gani ulitumia kukusanya takwimu zako na kufukia hitimisho kuwa kapuya ameonewa?
8. Kapuya amekanusha kuwa yeye hamfahamu huyo binti: Tarifa za kwamba wewe unafahamu uhusiano wa kapuya na huyo binti umezitoa wapi? cou
Katika wajinga we una digrii ya juu kuliko wooote super mbululaz kama unavyooita wengine. hivi wewe mzima kweli kichwani kwako? kwanza huna maana yeyote.wewe na kapuya ni sawa tuu.
Hata kama unayosema ni kweli lakini hujayathibitisha zaidi ya kuishia kusema sio kweli. Number ya Kapuya hata mimi nilikuwa nayo ni hiyo hiyo imetumika kutuma msg hilo vipi? You can cheat once but bot forever!
I know hii issue itazimwa hivi hivi. Lakini still Ana makosa kulala na mtoto wa umri mdogo no matter what especially mtu mkubwa wa umri , cheo, mume, baba, babu... Hii ni aibu kubwa! Na Kama alijijua Ana ugonjwa kwanini alilala nae bila kinga? Hilo ni kosa la jinai! Inabidi mahakama itoe tamko kwa daktari wake apimwe na wapate medical report yake.Kwa asilimia 97.5 naamini Kapuya kafanya hakusingiziwa na ni viongozi wengi tu huwa wanaonea kwa ajili ya power zao serikalini, ukifatilia kuhusu Kapuya Ana skendo chafu sana kwa wanawake ila nobody anakwenda foward kwa uoga wa kuuwawa na kadhalika inauma sana.
Huna loloteeee muongooo unaogopaaa umeshapigwa mkwalaaaa!! Mnafiki weweeeee!!!!
Huyu si ndio walewale!!!
Wewe siku zote nilisikia watu wakikusema Mutuz mtupu lakini leo naamini kabisa unamuombea radhi kapuya wewe kama nani yake Katibu wa chama chake,baba yake,mwanawe au rafiki yake?ikiwa katibu wa chama chake hakuomba radhi,unaomba wewe.number ya simu imeonekana ni ya kapuya amekiri namba yake,kigogo wa crdb pia katapeliwa na huo msichana..sio hoja,hoja kapuya kabaka hakubaka?mwisho sote wana CCM tunajua Kapuya muathirika mwaka wa ngapi sasa...angalia yako yakugombea ubunge achana na ya wenzako kwa faida yako
Mimi nadhani huyu mtu alioomba msamaha na kuweka picha yake. Ni mtu ambaye anataka cheap Popularity! Na umaarufu kwa ajili ya Ujinga! Kama wewe ni mtoa habari. Ilitakiwa kuwa na uhakika wa kile unachokiandika.
Lakini unasema ulikuwa mtu wa kwanza Kuandika na bila kuwa na ushaidi,Na sasa unakanusha bila kuwa na ushaidi.Na unaaapa Kwa mungu na kuomba msamaha bila kuwa na ushaidi. Naomba niulize umeishia Darasa la ngapi? Maaana umeingilia kazi ya Polisi,Mahakama,Na pande zote za Mashaidi. Kisa Mtu alikwambia kwamba huyo Dada ni muongo. Je Mtu Muongo habakwi? Angalia Maana ya kubaka au kubakwa, Haijalishi Muongo,Mkweli,mrefu, mfupi, Rangi,dini,inaweza kutokea kwa mtu yoyote, Je mtu mwenye mtoto haruhusiwi kuwa mwanafunzi? Na Hizo text zimetoka wapi na hiyo Ni ya nani. wote wanatakiwa ku-prove beyond reasonable doubt. ili tujue nani mkweli na nani muongo.Kabla kusema kwamba wewe ni kiongozi mkubwa wa ccm na Taifa. MIMI ni Mwana CCM Lakini nasikia aibu kubwa kuweka Ujinga kama huu na Kujitangaza kwamba ni Kiongozi wa chama. Siasa ni mchezo mchafu. Siasa za ushabiki zimepitwa na Wakati Ongea kitu Kinacholeta Maendeleo kwa Jamii na chenye Uhakiaka Safari yako katika siasa itakuwa Nzuri lakini kama ni Kigeu geu utaishia Kuwa bloger wa Katuni.
Nadhani Unatakiwa utuombe Msamaha watu tuliosoma article hii. Maana umetu- INSULT OUR INTELLIGENCE. Kwa kutuona wajinga!
You Make full of Your Self.How you involve in Politics. And Your this 0%Smart.!!!!
I hope your not support Division five too!!
Wewe ukiwa kama mmoja wa wanaondesha blog unayoiita Blog Ya Wananchi,unatakiwa uandike vitu vya kuwaelimisha wananchi sio UNAFIKI NA UMBEA,Hiyo blog yako ungeiita UMBEA BLOG,Umesha mwaribia Mtu jina lake Then you know that you can come up with your STUPIDITY Sorry,is not going to help anything,this is not the first time you come up with Stupid staff like that,your blog should be closed down... Unatumia jina la CCM na kusema unaelimu,wenye elimu hawafanyi UJINGA kama wewe,mbaya zaidi unaandika ujinga wako wote uliofanya...Chukua mifano kwenye blog ya MICHUZI Au VIJIMAMBO..
le mutuz jamani unamuombea msamaha kapuya kwa ajili gani au unataka kupata ubwabwa wako nawewe uwe ujiko katika ubunge, come on man yamekushindwa ya marekani unayarukiya ya kibongo bongo shauri yako tumia akili siyo hisia otherwise utapotea na watu watakusahau katika duru ya siasa kachini tafakari siyo unakurupuka wee na kuja hapa kuuza sura na ujinga ujinga wako shauri yako na unatuvalia hicho kikofia tukujuwe msomi mkubwa acha mikwara wewe hiyo degree marekani umepata ya nini si ya kutumia akili thats for really nakujua sana william poa bora kaa kimya fanya yako yanayokuhsu usitafute umarufu kwa njia hii
Muulize Uhuru1 alichosema kuhusu wewe kwenye post yako nyingine ya kumtetea Kapuya, mimi sijasema ila ninachokushangaa ni jinsi unatetea wanaume wapiga mpini, nini tatizo hapa???
Suala ni la Kapuya wewe umetoka wapi kumtetea, au wewe ni wakili wake hapa kwenye vijimambo??
Kakutuma??
Au umetumwa kwa niaba ya Kapuya kupitia Global Publisher???
Who are you kumtetea Kapuya??
Hebu tupe position kwa Kapuya then tueendelee mbele
Post a Comment