Kundi la P-Square la nchini Nigeria ambalo huundwa na mapacha Peter na Paul Okoye, leo limekutana na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kuzungumzia show yake ya Jumamosi hii Leaders Club.
P-Square wakiwa mbele ya waandishi wa habari, Dar
Akiongea kwenye mkutano huo, Paul alisema Tanzania ijiandae kwa show kali ya kwanza kufanyika baada ya kusherehekea siku yao ya kuzaliwa mwaka huu na wamekuwa wakijiandaa kwa show ya Leaders Club kwa kipindi kirefu. Paul Okoye (kulia) na Kelvin Twissa
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema kampuni ya Vodacom itaendelea kuunga mkono matamasha ya burudani nchini na kutafuta njia nyingi za kukuza muziki wa Tanzania.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa
“Kwa wasanii wa Tanzania hii ni nafasi yao kupata changamoto kuangalia kile ambacho ulimwengu wa muziki unachofanya, kuwa na vijana ambao ni Waafrika ambao wanavunja stage zote za dunia, wanavuka mipaka, ni kitu ambacho sisi tutakuwa tunafurahia sana,” alisema Twissa.
Mkuu wa East Africa Radio, Nasser Kingu
Bw. Harusi Peter Okoye akiongea na waandishi wa habariP-Square wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wengine wakiwemo Profesa Jay, Ben Pol na Joh Makini
P-Square wakiongea na wasanii wa nyumbani baada ya kuwasiliana kwenye mkutano na waandishi wa habari
Peter Okoye (kulia) akisalimiana na Profesa Jay na Ben Pol
Ben Pol na Profesa Jay
Bongo5
No comments:
Post a Comment