ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 22, 2013

KULIKUWA NA SHANGWE NA VIFIJO SIKU YA NDOA HII LAKINI SASA YAGEUKA NDOA NDOANO PINDU CHALI KULE

‘Thea’ na Mike Sangusiku ya ndoa yao.

Chanzo makini cha kuaminika kilichopo karibu na wanandoa hao kimesema ndoa hiyo ilivunjika rasmi Oktoba mwaka huu na sababu kubwa ikiwa ni kupigana mara kwa mara. “Unajua nyie mliandika ndoa imevurugika na Thea ameenda kwao eti atarudi watakapokaa na kuyazungumza, mmefichwa, Mike na
Thea wameshaachana na hakuna anayemhitaji mwenzake tena na Thea ameondoka na vyombo vyake vyote,” kilisema chanzo hicho.
Inadaiwa kwamba hata katika msiba wa dada yake Mike uliotokea hivi karibuni, Thea ingawa alikuwepo, lakini hakujishughulisha na lolote wala sare ya msiba hakuvaa na aliyeonekana kuchukua majukumu yake ni mke wa zamani wa Mike aitwaye Kuruthum Mpalu ‘Ummy’.

“Siku hiyo kila kitu kilikuwa wazi, mlishindwaje kubaini? Thea hakuwa karibu kabisa na alikuwa na mawazo tele, Ummy ndiye alikuwa ‘mother house’ na wengine wanadai amerudiana rasmi na Mike,” kiliendelea kutoboa chanzo hicho.
Kufuatia nyeti hizo, waandishi wetu walimsaka Thea na kufanikiwa kumpata bila hiyana akaweka mambo hadharani.

“Mh mnatafuta umbeya tu hapa, mimi nimeachana na Mike mbona siku nyingi tu, nyinyi ndiyo mnajua leo?” aliuliza.
Katika hilo, Thea alisema ana sababu nyingi zilizomfanya kuachana na Mike na kwamba baadhi yake hawezi kuziweka hadharani, lakini kubwa ni vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mwanaume huyo, kiasi kwamba ameshindwa kuvumilia kutokana na hasira alizonazo.

Thea alisema baada ya kuachana na Mike, ameamua kupumzika mambo ya wanaume kwa miaka miwili kabla ya kuamua vinginevyo maana ndoa hiyo imemchosha.
“Siwezi kusema sitaolewa tena, ila napumzika na ikitokea kuolewa itakuwa ni baadaye sana lakini katu sitarudi kwa Mike labda Yesu arudi,” alimalizia Thea.

Kwa upande wake, Mike alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu ndoa yake na Thea alikiri kuwepo kwa jambo hilo, akisema haelewi hasa kisa ni nini, lakini anaamini atajua baada ya muda siyo mrefu.
“Thea ameondoka kweli. Kuhusu siku ya msiba wa dada ni kweli Ummy alikuja na kunisaidia, lakini siyo kama tumerudiana isipokuwa yule ni mzazi mwenzangu na alijua kwamba Thea hayupo, ni hivyo.” Credit to GPL

No comments: