Ishu hiyo ilijiri huko Lagos, Nigeria ilikofanyikia sherehe hiyo ambapo Peter alifunga ndoa ya kimila na mrembo wa haja, Lola Omotayo huku Diamond akipata fursa ya kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa duniani, kasoro pekee ikawa kwenye mavazi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Diamond alichemka kwa kuvaa kivazi hicho kifupi miguuni kikiwa na mistari myeupe na myeusi hivyo kusababisha kutukanwa mitandaoni.
Emmanuel Adebayor (kushoto) na Diamond Platnumz wakiwa Four Point Hotel, jijini Lagos nchini Nigeria.
Huku wakitumia picha za waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond, Wema Isaac Sepetu na Jokate Mwegelo wakiwa wamevaa ‘taiti’ kama ‘kisuruali’ cha mwanamuziki huyo, walieleza kuwa inawezekana wao ndiyo walimdizainia hivyo kumsababishia matusi ya nguoni katika mitandao ya kijamii.
“Mafashenista wengi wanamtukana Diamond lakini inawezekana na zile nguo kadizainiwa na Wema au Jokate kwa sababu ni staili zao. Nao wana nguo kama hizo, hebu cheki kwenye picha,” alisema mmoja wa wachangiaji wa mada hiyo katika mitandao ya Naija huku akitundika picha za Wema na Jokate wakiwa wamevaa kama Diamond.
“Ni kweli Diamond amepata nafasi kubwa ya kukutana na mastaa wakubwa na kutangaza muziki wake kimataifa lakini kitu kimoja hakikwenda sawa.
“Ni juu ya nguo aliyokuwa ameivaa, mashabiki wengi wa muziki nchini Nigeria walisema kachemka,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni ya mashabiki wa muziki nchini humo.
Hata staa wa Nigeria aliyekuwa mmoja wa wenyeji wa Diamond, Iyanya alipoposti picha akiwa na Diamond pamoja na jamaa mwingine, ‘polisi jamii’ wa masuala ya mitindo waliendelea kugongea msumari wa moto kuwa Diamond akubali kuwa kachemka.
STAILI YA MICHAEL JACKSON?
“Iyanya, nani huyo kavaa suruali kama (marehemu) Michael Jackson? Mungu nisamehe kwa kukutenda dhambi lakini ukweli hicho kivazi hakiendani na mwili wake,” alifunguka shabiki mwingine kwenye ukurasa wa Iyanya wa Instagram.
Mwingine alisema: “Najua amekopi kwa mtu wake anayemhusudu (Wema), alionekana amependeza alipovaa hivyo walipokuwa China. Ukweli (Diamond) hakupendeza au labda kachukulia kwa Jokate wa Kidoti?”
ANGEENDA KUBADILISHA
Baadhi ya mashabiki hao walidai kuwa Diamond alipaswa kugundua kuwa yupo tofauti na mastaa wengine ili arudi hotelini mara moja akabadilishe nguo.
“Sijui alifikiria nini alipovaa hivyo, ona sasa amewaangusha na kuwadhalilisha mastaa wa Tanzania huko Afrika Magharibi.
“Ukweli ni kwamba kama alimuiga Wema na Jokate kachemsha, ona sasa wamemponza kwa kuvaa njiwa ya zebra kama wao.
“Diamond anajua kuvaa sana lakini anapaswa kuwa na dizaina wa kumpa ushauri wa mavazi kabla ya kwenda kwenye shughuli kubwa kama ile,” aliandika Mtanzania aishie Nigeria.
KAPATA ‘KIKI’?
Katika kujitetea huku akiamini kapata ‘kiki’ nchini Nigeria, Diamond alitumia ukurasa wake wa Instagram kwa kutundika picha yake akiwa na kisuruali hicho akiambatanisha na mastaa wakubwa wa Marekani kama akina Wiz Khalifa wakiwa wamevaa njiwa kama yeye kuonesha kuwa ni fasheni ya ‘mbele’.
Hata hivyo, hiyo haikusaidia kwani mashabiki hao waliendelea kumponda na kumtaka kujipanga zaidi siku akipata fursa kama hiyo kwani mastaa aliojifananisha nao walivaa hivyo katika ‘iventi’ tofauti na harusi.
MAMODO WANASEMAJE?
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya mamodo maarufu wa Kibongo ambao walishuhudia vazi hilo ambapo walikuwa na haya ya kusema:
“Sijui ni nani aliyemdizainia lakini kilichofanyika ni kwamba alimvalisha Kimarekani, akasahau kuwa alitakiwa amvalishe Kiafrika au Kitanzania. Unajua harusi yenyewe ilikuwa ya kimila haikutaka Umarekani hata kidogo ndiyo maana watu walimponda Diamond. Naamini wakati mwingie aliyemvalisha atafanya vizuri,” alisema modo maarufu wa Kiume Bongo, Martin Kadinda.
“Unajua mitindo ya mavazi unaweza ukatulia, ukadizaini kitu lakini ukifika mbele za watu wakakushangaa, hiyo ndiyo fasheni ilivyo. Simlaumu Diamond wala sisemi alitakiwa ashone khanga au kitenge lakini iwe changamoto kwa mamodo wetu waongeze ubunifu,” alisema modo mwingine.
Pamoja na mambo mengine, safari ya Diamond nchini humo ililenga kwenda kufanya kolabo na mastaa wawili wa Nigeria, Davido na Iyanya. Credit to GPL
No comments:
Post a Comment