ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 22, 2013

KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA"- Mwigulu Nchemba


Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu.
Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.

Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.
Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.
I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni.
Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi

12 comments:

Anonymous said...

Wacha unafiki wewe Nchemba:( Chadema chama makini... Zitto amekwisha kisiasa... Mchukueni huko CCM !

Anonymous said...

Hivi huyu mwigulu nchemba anajua maana ya think tanks?

Anonymous said...

Nadhani akili ndogo pia hutoa pumba nyingi kuliko ifanyavyo akili kubwa kwa sababu akili ndogo haina uwezo wa kuchumbua kipi kisemwe na kipi kisisemwe kwa audience. Nitaacha audience iamue kama Nchemba ana akili ndogo au akili kubwa!

Mdau

Anonymous said...

Mienendo ya Zitto haihitaji akili nyingi kufahamu alishapoteza muelekeo ...Hongera Chadema kwa uvumilivu wenu juu ya Zitto... Nimatimaini yetu kuwa atapata somo na kufanya uamuzi wa busara juu ya ukurasa wake mpya kisiasa... Kama kweli Zitto ni msafi tutaona kuanzia Leo na kuendelea!! Tuonyeshe usafi wako Zitto siyo kulumbana na Chadema... Toka na tuonyeshe nguvu zako nje ya Chadema kama kweli wewe ni msafi.

Anonymous said...

huyu mchemba chizi.

Anonymous said...

Mh. Nchemba, una akili kubwa sana homeboy! Umetusaidia sana kujua sababu zinazoisababisha CCM kuwanyamazisha wabunge wake wenye akili kubwa. Imewavua madaraka wengi na hata baadhi yao kuwafukuza uanachama. Hazijapita siku nyingi sana tangu Mzanzibari mmoja aonjeshwe joto hiyo ya jiwe. Sitakoma kukupigia kura homeboy!

Anonymous said...

Chadema kwisha habari,kama mmumemfukuza Zitto,Cdm itabaki historia,ubaguzi wenu na udini wenu unatufanya tuwachoke.kabisaaaa! Likadi lenu nimeshalichanana,that's it. Nimewatetea but kwa hili la Zitto, hapana. I'm pissed!!!!

Anonymous said...

Mwigilu, tunakufahamu sana na mambo yako tumeyaweka, sidhani kama unajua nini maana ya ulilotoa. Huna jipya kabisa kwani kwenye siasa wewe nawe umelimbikizwa. Nilikusoma ulipofanya safari ya America miezi michache iliyopita ulitakiwa kukaa chini na kujifunza zaidi. Acha hizo.

Anonymous said...

zito alishapotea kisiasa.sio mwanaharakati.yeye alijua yuko juu ya chama na nimaarufu kuliko chama.hongera CDM kwa kuonyesha ukomavu kisiasa.achana na nchemba wao ccm wamezoea kulindana.wanashindwa kukamata majangili.

Anonymous said...

Zito nakukubali ni mchapakazi usife moyo utafanikiwa kaka.kaza buti.

Anonymous said...

Kaka Zitto,the real patriots are behind you 120%,nchi bado inakuhitaji sana,either with Chadema au without Chadema,don't ever back down,wengi wetu tunakuombea!!! Fighters never lose!! If u love peace,then work for justice. And that's exactly.what u r doing!!! Thank u sooooo much!!!!

Anonymous said...

Wazulu wana wimbo wao maarufu unaoitwa Ayesab Amagwala(Waoga wanaogopa).Chadema ni Chama cha Kisophist(Wasomi wa Falsfa Wananielewa),Zitto si Mfuasi wa Itikadi hiyo ambayo ndiyo iliyoipa Chadema Ummarufu,ingawa nae aliitumia lakini aliiacha kwa sababu ya Mahaba kwa Tanzania na ndio sababu ya kuonekana ni Msaliti.kwa Zitto, siasa za uongo,chuki, ulaghai na kuchezea hisia moyo za vijana kwa kuwapa matumaini hewa ili wahamanike na kuwafia kina Slaa na Mamluki wengine kama Lissu kwake ni Siasa Haramu na alizipinga kwa vitendo na alisema kweli pale inapobidi.waoga wakaogopa nyendo za Zitto kukifanya Chama kuacha siasa za Kisophist zilizokipa umaarufu kwa huko ni kukiua Chama,na kweli kinakufa.Mh. Zitto"What Comes around,goes around" pole kwa kutafunwa na ulichokianzisha.nakuheshimu sana brother