ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 4, 2013

LOWASSA ANGURUMA BUNGENI


Edward Lowassa.

Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.

Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.

Aliwapongeza mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa barabarani badala ya kufanya kazi.

No comments: