Mchumba wa Luteni Mlima(watatu toka kushoto) akimliwaza mtoto wa marehemu aliefika kutoa heshima za Mwisho za Baba yake.
Pia, alisema kauli hiyo ndiyo ya mwisho kuisikia kutoka kinywani mwa mchumba wake huyo aliitoa baada ya kutolewa amri ya kijeshi kwamba anatakiwa kwenda kuwasaidia wenzake waliokuwa kwenye mapigano na askari wa waasi wa M23.
Askari huyo wa(JWTZ), Luteni Rajab Ahmed Mlima, aliuawa akiwa kwenye uwanja wa mapambano na vikosi vya askari wa waasi wa M23 katika milima ya Gavana, karibu na Goma, DRC wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana nyumbani kwake, Luteni Asia alisema, “Ninachokumbuka walitakiwa kwenda kuwasaidia wenzao waliokuwa kwenye mapigano kwa muda mrefu, tayari walikuwa wamezidiwa nguvu na askari wa waasi wa M23, ukweli hali ilikuwa mbaya na mimi nilimkataza asiende kwa kuhofia usalama wake,” alisema Luteni Asia huku akibubujikwa machozi.
Alisema wakati akimsihi asiende alimjibu kwamba ni lazima aende kuwasaidia wenzao, kwani kazi waliyotumwa kuifanya ni pamoja na hiyo hivyo asingeweza kuacha kwenda.
Aidha, Luteni Hussein alibainisha kuwa baada ya kwenda kutoa msaada na kufanikiwa kuwadhibiti waasi, muda mfupi baadaye alipata taarifa kuwa Luteni Mlima amefariki kwa kupigwa risasi jambo lililomshtua kiasi cha kuishiwa nguvu kabisa.Kusoma zaidi bofya
Alisema kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa, yeye anamwombea huko aliko apumzike kwa amani kwani amefariki akiwa anawatetea wananchi wa DRC na kuiwakilisha nchi yake.
Mipango ya harusi
Akielezea mipango yao ya harusi, Luteni Asia alisema Desemba 28, mwaka huu walipanga kufunga ndoa na kwamba taratibu zote zilikuwa zimekamilika ikiwa pamoja kutolewa mahari.
“Kwa kweli jambo linalo niuma sana na siwezi kusahau ni kwamba, tulikuwa tumebakiza muda mfupi tufunge ndoa na kila kitu kilikuwa kimeshakamilika hadi ukumbi wa kufanyia sherehe ya harusi yetu tulishaulipia,” alisema Luteni Hussein huku akibubujikwa na machozi.

2 comments:
Jamani pole dada maana yote ni mipango ya mungu, its so painful kumpoteza soul mate wako tena at the time you were waiting kuanza maisha pamoja. Ya-allah mpuzishe ndugu yetu na umsamehe madhambi yake yote. Ameen
POLE SANA MPENDWA HAKUNA WAKUKUPA FARAJA YA MOYO ZAIDI YAKUMTEGEMEA MUNGU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU ULICHONACHO.
Post a Comment