ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 4, 2013

NIMEMJUA MWANAMKE ANAETEMBEA NA MUME WANGU, NIMEUMIA SANAAA...!!

Naombeni msaada wa maawazo yenu, nimegundua kuna mwanamke anatembea na mume wangu, mume wangu alikataaaaaa kwa mara ya kwanza, lakini baada ya kufatilllia na kuchunguza kwa muda mrefu nikaja kuhakikisha ni kweli kabisa, mwanamke anaomba msamaha kwamba wataachana na hatorudia tenaa, na mume wangu pia anasema hatorudiaa,
Nimeumia sana mwenzenu, nimeumia kupita kias, kwakuwa nilimpenda, nilimheshimu, nilimjali sana mume wangu, nilikuwa teyari kumuachia yeye kila kilicho changu, nilimsikiliza sana, sikutegemea kama atakuja kunitenda hivi, imekia kipindi najuta kwanini niliolewa nay eye, sikutegemea kabisa kutokana na muonekano alio nao,,, details zoote za huyo mwanamke wake niko nazo, niliomba niprintiwe kupitia mitandao ya simu wanayotumia, niko nazo mkononi, staki kuamini, ninalia kama mtoto mdogo, ni bora niibiwe pesa nitatafuta, kuliko kuibiwa penzi,, nitalipata wapi,, 

Nimechanganyikiwa, nataka kuondoka kwenda kwetu nikapumzike, nimwache kwanza, maana kila nikimuona Napata hasira natamani kumkaba kabisa, nimemchukia mno,,, sina amani ya kuwa nay eye, hali hii hadi lini?? Nifanyaje?

7 comments:

Anonymous said...

i am selling my old gun .... :-)

Anonymous said...

Hafai huyo mwananmume. Mpige dafrao aende zake, atakuletea nayasiyotakiwa.

Anonymous said...

wanaotembea na waume za watu ni trash,na wengi hawana elimu na kuwaita hao wanaume kaka!!!! siku itakuja kuwarudia na kubaki bila hata rafiki. Kila kitu kina mwisho wake.

Anonymous said...

Pole sana dada, najua inauma sana hasa kwa mtu unaempenda na kumheshimu, hayo ni majaribu tu ya mwovu shetani hivyo hebu usimuache ashinde km mumeo amekuomba msamaha na ni mara ya kwanza kukufanyia hivi hebu try to give him a second chance, itakuwa ngumu kurudisha imani km uliyokuwa nayo mwanzo ila km unaamini ktk maombi basi hebu mlilie yesu na atakupitisha katika hili, mm sikujui ila nitazidi kukuombea. usikate tamaa dada.

Anonymous said...

Nakushauri kama amekuomba msamaha na kukiri kosa lake na atabadilika msamehe na uanze naye upya hapo ndio utakuwa na amani japo si rahisi ila ndio maana kwenye kufungishwa ndoa wanawauliza mtavumiliana katika shida na raha? Mpe nafasi nyingine ila ajirekebishe. Pole sana.

Anonymous said...

Hayo ndo yanayokusibu kuamua kufuatilia ungeliachana naye ukaanza zako mpya. Angalia unaweza kuwa wewe ndio chanzo kwani wengi wa wanawake ni miropoko mingi na kutataka kuwa na rafiki. Pole sana dada. Muweke pembeni kwa muda uangalie ustaarabu wako,

Anonymous said...

Ongeza utundu kitandani, hataenda popote, dada! But I know how you feel!