Na Mayasa Mariwata
MSANII wa filamu Bongo, Deogratus Shija ameshauriwa amuoe msanii mwenzake, Wastara Juma aliyekuwa mke wa rafiki yake, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, baada ya kufunguka kuwa hajampata mwanamke aliyetulia.
Ushauri huo uliibuka kwenye mtandao wa Face book hivi karibuni ambapo, awali msanii huyo aliandika ‘status’ iliyoeleza sababu za kutooa mapema licha ya kuwa umri unamruhusu ndipo wadau walipoanza kumshauri amuoe Wastara.
Mdau mmoja aitwae Milian Kopa alitupia ujumbe usemao:
”Muoe Wastara Shija, ya nini uhangaike wakati kila mmoja anatambua yule ni mke mwema.” Shija hakufunguka chochote juu ya ushauri huo ulioungwa mkono na wadau wengi.
No comments:
Post a Comment