BARUA YAKE YA KUJIUZULU:
Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA)
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.
Said A Arfi (mb)
3 comments:
chadema kimekuwa chama cha kikanda zaidi lazoma utoke Arusha au Moshi yaani kwa ufupi uwe mchagga ndio uweze kuwa na nafasi chadema, Zitto kuanzia aseme anataka kugombea urais imekuwa shida kwani hapigiwi kura ni lazima mtu ateuliwe ndio agombee kwa tiketi ya chadema?
Walichofanya CDM sio siasa mpya nchini Tanzania. CCM inaongoza kwa siasa kama hiyo. Asiyejua aongee na Maalim, Shibuda, na wahanga wengine wa aina hiyo.
Ndg msemaji usiwe kama Nchemba jifunze kufikiri la kuongea. Si kweli Chadema ni chama cha Wachagga unayo staristics ya usemalo tafadhali tumia wasomi wakusaidie kukupa taarifa sahihi. Chadema iko nchi nzima kote huko viongiozi wake ni Wachagga? Plse think before you lip.
Post a Comment