MATATIZO KWA MGONJWA WA SICKLE CELL
Mtu anapokuwa na ugonjwa wa Sickle cell damu yake hupungua sana na kushindwa kusafiri katika mirija midogo midogo ya damu mwilini mwake.
DALILI ZA UGONJWA
Mtu mwenye Sickle cell anaweza kusikia kupooza mwili, miguu na tumboni na anaweza kuambukizwa kirahisi magonjwa.
Mgonjwa anaweza pia kupata vidonda vidogo vidogo kwenye miguu ambavyo hataweza kujua vimetokana na nini.
Mgonjwa mwenye maradhi haya kama ugonjwa utatokea, mapafu yake yatashindwa kufanya kazi ipasavyo hivyo kusikia maumivu makali kifuani ambayo kitaalam huitwa Acute chest syndrome.
Tatizo lingine ambalo mgonjwa atapata ni figo zake kushindwa kufanya kazi kutokana na kuathirika ama maji kupungua mwilini, hivyo mgonjwa kupata tatizo la kutopata mkojo sawasawa.
Mgonjwa pia atakuwa na tatizo la hatari la damu yake kushindwa kwenda kwenye ini, tendo ambalo kitaalam huitwa Sequestration.
Wanaume ambao ugonjwa huu umewaathiri watakuwa wakisikia maumivu kila mara watakapokuwa wanasimamisha uume kitendo hicho kitaalam huitwa Priapism.
Wagonjwa wengi wenye Sickle cell macho yao huathirika na kuwa na kiwango kidogo cha chembechembe za damu (Red Blood Cell) mwilini.
Mtu ambaye amekuwa na ukosefu wa chembechembe nyekundu za damu huwa ni rahisi kwake kukumbwa na ugonjwa wa Anemia.
Ugonjwa huu ikiwa utampata mtoto mchanga basi ukuaji wake utakuwa wa taratibu sana ukilinganisha na watoto wengine ambao hawana maradhi haya.
Matibabu, ushauri
Ukiona dalili kama hizi tulizozitaja zinakutokea mara kwa mara, muone daktari mara moja naye atakupima damu yako kubainisha iwapo una huo ugonjwa au la.
Daktari wako akigundua kuwa unao atakupatia dawa pia atakupa ushauri wa vyakula ambavo utakuwa ukitumia hasa mboga za majani kwa wingi, samaki, dagaa, maziwa na matunda ambayo yatakusaidia ili tatizo hilo lisikudhuru kwa kiasi kikubwa.
Wapo watu wanaishi muda mrefu kwa kufuata masharti na wakaishi bila kusumbuliwa na tatizo hili la kupungukiwa na damu mara kwa mara baada ya kufuata masharti.
GPL
No comments:
Post a Comment