ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 12, 2013

KANISA THE WAY OF THE CROSS MINISTRIES LA COLLEGE PARK, MARYLAND LAPATA BASI DOGO

Kanisa la THE WAY OF THE CROSS lililopo College Park Maryland nchini Marekani jumapili Novemba 10, 2013 lilisherehekea uzinduzi wa gari lake (Van) kwa ajili ya usafiri wa waumini na watu wote wanaohitaji kwenda kupata huduma za kiroho kanisani hapo.
Mchungaji Ferdinand Shideko wa kanisa la The way of the cross akisoma neno ambalo lilikuwa ujumbe juu ya uzinduzi wa gari la kanisa hilo hapo juzi november 10 katika viwanja vya kanisa hilo huko College Park Maryland.
Mchungaji Ferdinand Shideko akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Van la kanisa.
Waumini wa kanisa la The way of the cross wakiimba na kucheza ikiwa ni furaha ya kupata gari la kusafirisha kanisani na kuwarudisha makwao
Shangwe zikiendelea, ilikuwa ni furaha tupu!
Ferdinand Shideko Mchungaji wa kanisa hilo la The way of the Cross sasa akiwa ndani ya gari hilo kujaribu kuangalia 'Je linaWaka'
Mchungaji John Mbatta akiomba maombi ya shukurani kwa upatikanaji wa gari hilo la kubebea waumini.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo Amos Cherehani akitoa maelezo machache kwa waumini kabla ya shughuli ya uzinduzi kuanza

No comments: