MILLARD AYO
Katika pitapita zangu mtandaoni nkakutana na story hii kutoka MO BLOG nikasema si vibaya nkiwajuza wasomaji wa VIJIMAMBO Blog kuhusu story hii ambayo wengi hawaijui kuhusu Millard Ayo.
MO BLOG: Hebu Millard tufafanulie zaidi tukio hilo la ajali lilikuaje..?
MILLARD AYO: Yaani sina la kusema ila kama Mungu asingependa mimi nisingekuwepo duniani, lakini kwa sababu alipenda, ndio maana nipo, hata hili kovu katika kichwa upande wa kushoto lipo. Hapa iliingia chuma, unajua mabasi ya zamani yalikuwa na chuma, sasa ile chuma ilikatika wakati basi likijipiga kwenye mawe kama unavyojua kule ni crater.
Kwa kweli ninachokumbuka ni kuwa gari lilipotulia watu walikuwa wakilia na damu zinatiririka na mimi nilikuwa nimebanwa katika hiyo chuma na nilipotolewa sikukumbuka tena nini kiliendelea.
Ilikuwa mbaya sana kwa sababu lile basi lilikuwa likibiringika kama chupa, hivyo watu wanatupwa madirishani na kisha gari linawalalia ndio mazingira watu walivyopoteza maisha.
OMG…!!!
No comments:
Post a Comment