KWA mujibu wa wataalamu na watafiti wa masuala ya afya ya mwanadamu, zama za matumizi ya dawa za ‘antibiotic’ zinazoaminika kutibu magonjwa mengi ya kuambukiza, zimeanza kutoweka baada ya dawa hizo kubainika kukosa uwezo wa kuua vijidudu, licha ya ukali wake.
Baadhi ya watumiaji wameanza kubaini ukweli huu baada ya kujikuta wanatumia dawa hizo kwa wingi bila kupata ahueni ya matatizo waliyonayo, badala yake wamejikuta wakipatwa na madhara mengine ya kiafya, hasa kwa akina mama ambao huambukiza watoto walio tumboni na athari zake kuonekana mtoto anapozaliwa.
SABABU ZA HALI HII
Kuna sababu kadhaa za dawa kuishiwa nguvu, chache kati ya hizo ni pamoja na ukweli kwamba kuna aina nyingi za bakteria sugu ambao wanabadilika kila kukicha na kwa kasi ya juu kuliko utafiti unaofanywa na wataalam kuboresha dawa hizo.Aidha, makampuni mengi yanayotengeneza dawa hizo, baadhi yameacha kuvumbua aina nyingine ya dawa za ‘antibiotic’ za kuendana na mabadiliko ya bakteria, sababu ya kuacha kuendeleza dawa hizi ni faida ndogo wanayoipata kwa aina ya dawa hizo.
Utakumbuka kwamba makampuni mengi ya dawa yako kibiashara zaidi kuliko kuokoa maisha ya watu, hivyo yameacha kuendeleza utafiti wa dawa hizi na badala yake yamejikita kwenye kutengeneza dawa zenye faida kubwa kama vile dawa za saratani, magonjwa ya moyo, kisukari, presha na ukosefu wa nguvu za kiume!
Kwa muda mrefu zimekuwepo makala kadhaa kwenye magazeti na majarida ya afya duniani yakitahadharisha madhara ya dawa za ‘antibiotic’, lakini Dr. Ajun Srininasan ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC), anasema kuwa hivi sasa mwisho wa ‘antibiotic’ umeshawadia na hatuna njia nyingine zaidi kutumia njia asilia za kujikinga na maradhi.
NINI CHA KUFANYA?Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa, kuna njia nyingi za kufanya ili kujikinga na maradhi. Kwa sababu tutakuwa hatuna chaguo lingine, pengine sasa ndiyo wakati muafaka wa kuzijua na kuzitumia njia hizo, ambazo zaidi zinahusisha ulaji wa vyakula sahihi.
Mungu ameumba kila aina ya vyakula na kila kimoja kina kazi na faida yake mwilini. Vyakula vinavyoaminika kuwa na virutubisho asilia sawa na vile vya dawa za ‘antibiotic’, ni pamoja na kitunguu saumu (garlic), mdalasini (cinnamon), asali (honey), mwanga wa jua na vitamin D. Upigwapo na mwanga wa jua la asubuhi unajipatia vitamin D mwilini ambayo ni moja kati ya vitamini zinazodumisha kinga mwilini.
Mwili ukiwa na kinga ya kutosha, siyo rahisi kupatwa na maradhi ya kuambukiza na yale ya mlipuko, kama uvimbe, vipele, kifua kikuu, mafua ya muda mrefu, saratani, n.k. Ili kuupa mwili uwezo wa kujikinga wenywewe, unatakiwa kuzingatia suala la kula matunda, mboga za majani, hususan vitunguu na nyanya aina zote bila kusahau suala la kufanya mazoezi.
Aidha, ukiwa na kinga imara asilia, hata inapotokea ukalazimika kutumia dawa za ‘antibiotic’ zitaweza kufanya kazi kama kawaida, kwani usugu wa vijidudu huimarika zaidi pale kinga asilia inapokosekana kabisa mwilini. Kwa maana nyingine, usugu wa vijidudu huimarishwa zaidi na mwili wenyewe.
GPL
No comments:
Post a Comment