Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya karage suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu Fadhili awadh[tiger] katika uzito wa wealter[66kgs] pambano la raundi kumi, nao wanategemea kupima hiyo kesho
kizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa mabondia wanaotegemea kupima ni mbaruk heri mabae atapima kwa ajili ya kuzipiga na lusekelo daudi ,Issa omar nampepeche na Hassan kiwale’moro best’, Zumba kukwe na Jacob maganga, Adam Yahaya na Harman shekivuli, jocky hamis na mbena rajab, Ernest Bujiku na Shah kasim, shaban bodykitongoji na mwinyi mzengela, shaban manjoly na kasim chuma.
Nae Mtanzania aishie Canada kareem kutch atapima na Tata boy kwa ajili ya pambano la kimataifa la mchezo wa kickboxing la raund tano, Mabondia wote wameshawasili Dar es salaam, wakati Alibaba Ramadhan wa Arusha na Jacob maganga wa Tanga wamefikia katika hotel ya valley view wakati kareem kutch yupo Durban hotel kariakoo wapo vema na wenye furaha kwa mapambano yao
No comments:
Post a Comment