Advertisements

Monday, December 2, 2013

KATIKA MAFANIKIO YA DIAMOND, UCHAWI NA WANAWAKE VYATAJWA KAMA NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO YAKE..!!

MEBAINIKA kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,Nassib Abdul Mohamed maarufu kwa jina la (Diamond Platnumz) anatumia nyota za wanawake katika kujipatia umaarufu, habari za ndani zinazomhusu msanii huyo zinadai kwamba amekuwa akitumia nyota za wasichana mbalimbali nchini kujipatia umaarufu.
Taarifa za ndani zilizonaswa na Papaprazi wetu kutoka kwa watu wake wakaribu zinadai kwamba msanii huyo ana amini katika ushirikina na kwamba anamganga wake wa kienyeji anayemtengezea nyota yake, kutokana na nyota za wasichana anao kuwa nao kimapenzi, ambapo anatumia nguo zao za ndani ,leso zao za kujifutia jacho pamoja na picha zao za kiganjani.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya Diamond kupeleka vitu hivyo kwa mganga wake, ambaye huviingiza katika luninga yake na kupiga ramri yenye nguvu ya kutambua nyota za msichana husika, baada ya hapo Diamond hudumu na msichana huyo mpaka atakapobaaini kwamba amekomba bahati zake zote kisha anatafuta sababu za kumuacha.

"Diamond hafai kabisa ni mshirikina ni mchawi, anaroga watu hususan wanawake,Diamond akikutaka kimapenzi ujue kwamba ukiachana naye lazima ufirisike ama uyumbe na kama ukiwa maarufu lazima umaarufu wako uporomoke, epu fanya utafiti kuanzia kwa wasicha wote aliowahi kutembea nao, tangu alipopata umaarufu mfano, alipokuwa na Wolper kila mtu anajua maisha ya Wopler pamoja na umaarufu wake ulivyokuwa,mtizame Wolper alivyo hivi sasa kama vile kachanganyikiwa"kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania Diamond Platnumz
"Mtizame Jokate wakati akiwa na Diamond maisha yake yalikuwaje, Jokate alikuwa na maisha ya juu lakini tangu alipoachana naye tu mambo yake yakaanza kuyumba, kuliko alivyokuwa awali, mtu mwingine ni Penny ambaye ni mtangazaji wa Luninga ya DTV, yule demu ukimwona hivi sasa huwezi kuamini, kwanza amechanganyikiwa kabisa, mtu mwingine ni Wema Sepetu kila siku ni majanga, inasemekana kwamba nyota ya Wema bado ina nguvu kwa Diamond kuliko wanakwake zake wote, lakini kwa masharti ya mganga wake ni kukaa na kila msichana kwa muda usiozidi miaka miwili ndiyo maana Wema bado anamuota Diamond hadi leo".

Hata hivyo Chanzo hicho kilidokeza kwamba, msanii huyo amegonga mwamba kwa Lulu kwa sababu Lulu hivi sasa anadaia kuwa na mtalaam mmoja mkali anayemtengenezea mambo yake, tangu alipo haribu nyota yake kutokana na kifo cha Kanumba na kwamba moja ya masharti yake kwa sasa ni kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa sababu msanii huyo ndiye aliyempa mikosi tangu alipokuwa na Kanumba.

"Kama utakumbuka vizuri siku ya ugonvi wa Kanumba na Lulu kabla ya kifo kutokea Lulu alikuwa na ahadi ya kukutana na Diamond na akawa na mipango ya kutoroka usiku lakini kwa kuwa jamaa alishtukia mpango wake akawa anajaribu

5 comments:

Anonymous said...

Hivi wewe uliyeandika hii habari una akili kweli? Mbona una wivu sana, nadhani wewe ndo mshirikina. Kwanza unaandika uwongo mtupu hivi kweli Jokate, Wolper wamefirisika??wewe ndo umefirisika kiakili. Unapewa habari na wavivu wenzako wa kufikiri.

Anonymous said...

I agree. Watu wengine mmedanganyika na waganga waganga. Muacheni Diamond aendelee kushaini. Sasa waliofanikiwa kwa muziki ughibuni wanaenda kwa waganga gani???? Tumieni akili unless unataka kuuza hizi habari upate kidogodogo cha chai! Grow up people acheni kuendekeze ujinga.

Anonymous said...

jamani Wa TZ tukue kiakili, na tuwe na uwezo wa kufikiria kabla ya kusema au kuandika jambo. Mimi nafikiri aloaandika hiyo mada ya diamond yeye ndio mshirikina kaenda kwa waganga wake huko kwa nia ya kutaka kumchafulia diamond ndio akazuka na hayo mambo ya kutaka kumchafulia diamond jina.Wa TZ tuache wivu wa kijinga, na wewe uloandika kuhusu diamond wacha uvivu kachakarike kama mwenzio. KEEP IT UP DIAMONG. haya majungu yasije yakakurudisha nyuma.

Anonymous said...

Mmmmmh jamani huwa nacheka saana WATANZANIA wanapojifanya kana kwamba hawajui au hawakusikia UCHAWI!! Mhhhhhh ACHA UONGO! kuna watu usiku hawalali hapa DMV kwa kuwanga VIGAGULA VILE!

Anonymous said...

Kimbaumbau wa mtaa wa pili oyeeeeee kwa kuwanga!!