ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 30, 2013

MAUWAJI YA KINYAMA IRINGA MWANAMKE AUWAWA KWA KUCHOMWA VISU MMOJA AJERUHIWA VIBAYA

Waombolezaji wakiwa katika msiba huo eneo la Mtwivila 
Mume wa marehemu Bw Hamza Kidava na mtoto wake wakitoa heshima za mwisho kabla ya mazishi 
kwa picha zaidi na maelezo bofya soma zaidi
mwili wa marehemu Doris Lyandala
Kaburi la marehemu Doris
Aliyekuwa mume wa marehemu Doris Lyandala Bw Hamza Kidava kushoto akiwa na rafiki zake nyumbani kwao Mtwivila leo
Bw Hamza Kidava akiwa katika majonzi mazito
Bw Hamza Kidava akionyesha eneo ambalo mke wake kipenzi alipouwawa kwa kuchomwa visu na mtu anayesadikika kuwa ni kichaa
Bw Hamaza kushoto akimwonyesha mwandishi wa mtandao huu mzee wa matukio daima hayupo pichani na Bw Brown eneo ambalo mke wake aliuwawa
Dereva Taxi aliyekuwa akimwendesha Mzee wa matukio daima Bw Brown akiwa nje ya nyumba aliyekuwa akiishi mtuhumiwa wa mauwaji ya Bi Doris Lyandala 


HAKUNA Kati yetu ajuaye siku yake na kufa na kifo chake kitakuwaje na kama ungelijua lijalo mbele yako hakuna ambaye angejaribu kutoka ndani ya nyumba yake kwenda kukutwa na mauti.
Ni kauli za majirani na marafiki wa karibu wa mrembo Doris Lyandala ambae kwa sasa kwa wakazi wa mji wa Iringa jina lake ndilo limeendelea kutesa mawazo ya wengi.
Doris ambae enzi za uhai wake alipata kuwa mmiliki wa Saloon yake ya kutengeneza nywele warembo wenzake na alipata kuwa mcheshi asiyependa makuu tulitamani tungekula na kusherekea nae pamoja Krismas ambapo ilibaki siku moja pekee kula Krismas na rafiki ,familia yake na zilibaki siku takribani 7 kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ila yote hayakuwezekana na badala yake rafiki na ndugu walijikuta katika simanzi ya kifo chake .
Mmoja kati ya marafiki zake wa karibu Salima Alli alisema kuwa alikuwa ni mteja wake mkubwa katika saloon na kabla ya kukutwa na umauti siku moja kabla alipata kumseti nywele zake.
Bw Hamaza Kidava ndie mume wa marehemu huyo anasema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kipenzi chake mke wa mtoto mmoja amepatwa na tatizo na amekimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa baada ya kufika Hospital hapo hakuamini kuona mke aliyempenda kuliko akitokwa na damu huku akieleza kwa shida kilichomkuta .
Akizungumza kwa uchungu mwigi huku akilengwa na machozi Hamza ambae ni mmoja kati ya vijana watanashati na wenye ajira zao akiwa katika sekta ya kutengeneza simu alisema kuwa alichoelezwa kuwa amechomwa visu na kichaa.
"Ina niuma sana kumpoteza mke wangu na ina niuma sana kuona leo nimebaki mpweke nikilea mtoto mmoja ambae nimezaa nae mke wangu Doris ....kaka nashukuru kwa kuja kunifariji na nawashukuru wote walioshiriki kuuguza hadi mazishi yake "alisema Hamaza kumaliza kwa kusema twende nikakuonyeshe alipokutwa na mkasa huo wakati akitoka dukani kutafuta mahitaji.
Ndudu wa karibu na mtuhumiwa wa mauaji hayo ambae hakupenda jina lake kuandikwa hapa kwa kuwa si msemaji wa familia alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji Bw Zakayo Lwambano (26) ni mkazi wa Mtwivila na alikuwa akiishi mtaa mmoja na marehemu Doris .
Alisema kuwa kijana huyo Zakayo alianza kuugua ugonjwa huo toka mwaka 2010 ambapo ndugu walimpeleka Hospital ya vichaa Milembe Dodoma na kurejea akiwa mzima wa afya.
Hata hivyo alisema baada ya kurejea alikuwa ni mtu aliyetulia na kujipatia kipato chake cha kila siku kwa kufanya kazi ndogo ndogo za kusomba mchanga na nyingine kwa wananchi wa eneo hilo .
Ndugu huyo alisema wazazi wa mtuhumiwa huyo kwa sasa walisha fariki dunia na alikuwa akiishi peke yake katika getho ( nyumba yake ya chumba kimoja ) aliyojenga mwenyewe
Alisema kuwa siku ya tukio Desemba 24 kabla ya kumshambulia Mrembo huyo alianza kumchoma kisu ndugu yake James Moyo (28) ambae alifika nyumbani hapo kwa ajili ya kula sikukuu akitokea Makambako Njombe.
Alisema kijana huyo aliyejeruhiwa alikuwa akiishi nyumba nyingine tofauti na getho la mtuhumiwa na alichomwa visu viwili kwapani na kukimbizwa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kwa sasa ameruhusiwa na kurejea Makambako kwao.
Pia alisema mtuhumiwa huyo baada ya mauwaji alijipeleka mwenyewe polisi na kutaka awekwe ndani kwa madai ameua
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kutokea kwa mauwaji hayo na kuwa mtuhumiwa huyo hadi sasa anashikiliwa na polisi .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa mwanamke huyo alichomwa visu sehemu mbali mbali ya mwili wake na baada ya kukimbizwa Hospital akiendelea na matibabu alifariki dunia.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo amenashikiliwa kama watuhumiwa wengine na kuwa mwenye mamlaka ya kumfunga ama kutomfunga ni mahakama na wao kama polisi hawajui kama ni kichaa wanajua kama mtuhumiwa wa mauwaji.
Mtandao huu na wadau wake unatoa pore nyingi kwa familia ya Kidava na Lyandala pamoja na ndugu na jamaa wote ambao wameondokewa na mpendwa wao ambae sote tulimpenda sana ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo hatunabudi kusema jina lake lihimidiwe milele yote



Chanzo;Fransis godwin blog

No comments: