Mike Shanahan
Meneja Mkuu wa timu ya football ya Washington Redskin Bruce Allen ametangaza kumfukuza kazi kocha wa timu hiyo Mike Shanahan. Bruce Allen ametangaza uamuzi huo leo alipokua akiongea na waandishi wa habari, meneja mkuu huyo wa Washington, Redskin amesema ulikua ni uamuzi mgumu lakini ilibidi wafanye hivyo kwa kuinusuru timu kufanya vibaya msimu ujayo na alipoulizwa kama waishapata kocha mwingine wanayetarajia kuwa naye msimu ujao, Bruce Allen amesema mpaka sasa msako wa kocha mpya unaanza usiku huu kuna majina ya makocha wanayo yapitia ili mazungumuzo yafanyike na hatimaye kuja na jibu kamili ya nani atakayekuwa kocha mpya wa timu hiyo kipenzi ya wengi maeneo ya DMV na majimbo mengine.
Mashabiki wengi wameonekana kufurahia kufukuzwa kwa kocha huyo ambaye anakuwa kocha wa nane tangia Dan Snyder anunue timu hiyo mwaka 1978
Mashabiki wengi wameonekana kufurahia kufukuzwa kwa kocha huyo ambaye anakuwa kocha wa nane tangia Dan Snyder anunue timu hiyo mwaka 1978
No comments:
Post a Comment